Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh,Paul Makonda ameshuhudia utiaji Saini wa ujenzi wa soko la kisasa la machinga eneo la Morombo jijini Arusha pamoja na ujenzi wa uwanja wa michezo

Aidha ujenzi wa soko hilo la kisasa utagharimu shilingi milioni 710,129,240.94 huku uwanja wa michezo utagharimu Bilioni 9,614,158,878,60

Katika miradi hiyo kampuni ya SUMA JKT Construction LTD ndio itakayojenga ujenzi wa soko jipya eneo la Morombo kata ya Muriet jijini Arusha,huku ujenzi wa uwanja wa michezo ukisimamiwa na kampuni ya STC Construction Ltd

Zoezi la utiaji saini ulifanyika juni 17,2025 ukishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali,vyama pamoja na wananchi wa eneo hilo

Aidha pamoja na utiaji saini wa miradi hiyo,Mkuu wa Mkoa Makonda amegawa pikipiki 23 pamoja na Bajaji mbili kwa Watendaji wa kata zote jiji la Arusha kwaajili ya kuwarahisishia katika shughuli zao za kila siku

"Fedha za kununua vyombo hivyo vya moto ni sehemu ya shilingi milioni 300 zilizotengwa na halmashauri ya jiji kwaajili ya kununua gari la mstahiki Meya"Anasema Makonda

Ameongeza kuwa toka ameingia Arusha amefanikiwa kusukuma miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa stendi ya mabasi eneo la Bon city,Soko la kilombero,Ukumbi wa mikutano,uwanja wa michezo,Uwanja wa mpira wa Afcon na ujenzi wa barabara za lami,

"Ifikapo Julai 1 mwaka huu miradi yote itakuwa imefikia hatua nzuri sanaa na mimi naona fahari kuona miradi hiyo inatekelezwa"Anasema Makonda

Kwa upande wake Meneja wa SUMA JKT,ujenzi Kanda ya Kaskazini, Luteni Kanali Mhandisi Daudi Zengo anasema wanatarajia kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa wa miezi sita ili shughuli za uzalishaji ziweze kuendelea

Pia alisisitiza kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia ubora unaotakiwa ili kujenga uaminifu kwa kampuni hiyo ya kizawa iliyopo chini ya serikali

Naye Meya jiji hilo Maxmillian Iranqhe anasema katika kipindi cha miezi sita Halmashauri ya jiji imeweza kusaini miradi ya zaidi ya bilioni 60 iliyotokana na jitihada za Mkuu wa Mkoa Makonda.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...