Na Mwandishi Wetu,Chato
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira, amezuru kaburi la hayati Rais Mstaafu Dk.John Magufuli, kama moja ya ishara ya kutambua mchango wa kiongozi huyo katika kuchochea maendeleo ya taifa wakati wa uongozi wake.
Makamu Mwenyekiti Wasira yuko mkoani Geita katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa chama, ambako kesho pia anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa daraja la Magufuli la Kigongo - Busisi, ambalo kwa mujibu wa taarifa za awali tukio hilo litaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...