-REA kuendela kuwajengea uwezo Magereza uendelezaji Miradi ya Nishati Safi

-Mhe. Balozi Radhia Msuya amewahamasisha Maafisa na Watumishi wa Magereza kuwa Mabalozi wa Nishati Safi

Serikali imesambaza kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza (Gereza la Ukonga) mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko yake 464 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama njia ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini ambapo msisitizo ni angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ifikapo Mwaka 2034.

Hafla ya ugawaji wa mitungi na majiko yake iliongozwa na Mhe. Balozi, Radhia Msuya, Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vjijini (REB) katika gereza la ukonga, Jijini, Dar es Salaam, leo Juni 30, 2025 ambapo kwa upande wa Magereza uliwakilishwa na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi, (ACP); Athuman Recha.

Balozi, Radhia amesema kuwa, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Watumishi hao watasambaziwa mitungi ya gesi na majiko yapatayo 464 na kuongeza kuwa huo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Awamu ya Sita; Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kama nyenzo ya kulinda afya za Watanzania, kulinda na kutunza mazingira

Amesema kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia makubaliano na Jeshi la Magereza ili kuwawezesha, kuhama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo salama kwenda katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika magereza yote nchini.

“Serikali kupitia REA, ilishaanza uwezeshaji kwa Jeshi la Magereza na wameshaanza kutumia Nishati Safi na kwa msisitizo huo, tuliona ni vyema, kuwawezesha Watumishi na Maafisa ili nao waachane na nishati chafu ili kulinda afya zao pamoja na kulinda mazingira yetu”. Amesema, Mhe. Balozi, Radhia.

Naye, Mkurugenzi wa Fedha na Uwezeshaji, CPA, Daniel Mungure ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), amewataka watumishi wa jeshi la magereza kuibeba Ajenda ya Mhe. Rais Samia ya kuwa Mabalozi wa Nishati Safi ya kupikia kwa kuendelea kutumia gesi na siyo kuni na mkaa.

Akishukuru kwa uwezeshaji huo kwa Watumishi na Maafisa wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi, (SSP); Moses Mumbi amesema, wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwajali na kuongeza kuwa teknolojia hizo za Nishati Safi ya Kupikia si tu zinalinda afya zao lakini zinaongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao wakati wa kuwahudumia Mahabusu na Wafungwa.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...