Na Vero Ignatus,Arusha

SERIKALI imeweza kuandaa jumla ya mipango ya matumizi bora ya ardhi 2,480 katika kipindi cha miaka minne ambapo vijiji 4,679 vimewekwa katika mipango hiyo kati ya vijiji 12,333 nchi nzima. 

Hayo yamesemwa Leo June 23 2025 Jijini Arusha na Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi,Mhandisi Anthony Sanga kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Deogratius Ndejembi wakati wa ufunguzi wa jukwaa la wadau kutoka sekta binafsi na serikali pamoja na wakuu wa wilaya mbalimbali wakijadili mipango ya matumizi bora ya ardhi. 

 Mhadisi Sanga alimshukuru Rais Samia kwa kuiongeza fedha Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ambapo jumla ya mipango ya matumizi ya ardhi 4,679 imeweza kuandaliwa kati ya vijiji 12,333 ambapo kwa sasa vijiji 7,654 vimesalia pasipo kupangwa. 

Aidha tangu kupatikana kwa uhuru serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha migogoro ya ardhi inapungua ikiwemo wakurugenzi wa halmashauri kuendelea kupima maeneo ya vijiji na kupanga matumizi bora ya ardhi angalau vijiji sita kwa mwaka mmoja katika kila halmashauri nchi nzima

"Hili ni jambo kubwa la kumshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa utoaji wa fedha kwa tume na kuwezesha vijiji hivyo kuwekwa katika mipango ya matumizi bora ya ardhi na kuwashukuru wadau kutoka sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali katika kupanga matumizi bora ya ardhi"

Alisema mipango ya matumizi bora ya ardhi inaandaliwa kutoka vijijini hivyo mipango shirikishi itaondoa migogoro mbalimbali ya ardhi ikiwemo migogoro ya mijini ambayo wananchi ni wengi maeneo yamebanana zaidi kutokana na wingi wa watu na kushauri maeneo ya vijiji kujenga nyumba za kwenda juu ili kupata maeneo mengine ya kilimo na shughuli nyinginezo ikiwemo viwanda ili kukuza uchumi

Ametilia mkazo kuwa wizara ya ardhi itaendelea kuuhisha ramani za msingi zilizokuwepo tangu miaka ya 70 zilizopo nchi nzima ili kuwa na ramani bora sanjari na ununuzi wa ndege na droni ikiwemo utoaji wa hati za kimila ikiwemo kuboresha vituo vya upimaji vya kieletroniki ili kurahisisha upangaji na upimaji wa miji na vijiji ikiwemo maeneo mengine muhimu kwa ustawi wa jamii

Akisoma taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi Joseph Mafuru , Dk, Joseph Paulo ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Matumizi Bora ya Ardhi alisisitiza wadau hao kushirikiana na tume kwaaajili ya kupanga maeneo ya vijiji na miji ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana ikiwemo kutenga maeneo ya malisho na mengine ya huduma za kijamii

Raymond Mangwala ni Mkuu wilaya ya Rombo ,  amesema wilaya hiyo inachangamoto ya ardhi kutokana na wananchi kumiliki ardhi kwa tamaduni za kimila lakini kuja kwa mpango huo wa matumizi bora ya ardhi umewezesha vijiji kupangwa vizuri huku vijiji 24 vikipimwa na kijiji kimoja kupata hati 

Vile vile  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema amesema wilaya hiyo ni kati ya wilaya yenye migogoro ya ardhi kutokana na vijiji 63 kukosa mipango bora ya ardhi na kusisitiza viongozi wa vijiji, wilaya na mkoa kuheshimu mipaka iliyopo ikiwemo kuepuka rushwa. 

Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhandisi,Mhandisi Anthony Sanga kwaniaba ya Waziri wa wizara hiyo, Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la wadau kutoka sekta binafsi na serikali,Wakuu wa Wilaya mbalimbali wakijadili mipango ya matumizi bora ya ardhi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...