NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

SHIRIKA lisilokuwa la kiseriki  la Room to Read katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu limewafikia na kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha na malezi wanafunzi  wa kike wapatao 679  kutoka Mkoa wa Pwani.

Aidha shirika hilo  limeishukuru kwa dhati  serikali  kwa ushirikiano ambao umefanikisha mradi wa Usomaji na Maktaba kwa baadhi ya Shule za Msingi  na kuwezesha kupunguza changamoto ya wahitimu kumaliza wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Hayo yabebainishwa na Mratibu wa Mradi Usomaji na Maktaba kutoka Room to Read  Dickson Msuva kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Msuva alisema kuwa mradi huo ambao uko kwenye baadhi ya mikoa kwenye shule hizo umewarahisishia wanafunzi kujua kusoma na kuandika kwa haraka kutokana na uanzishwaji wa maktaba mashuleni.

"Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano ambapo anzishwaji wa maktaba mashuleni kumesaidia kukabili changamoto ya wanafunzi kuchelewa kujua kusoma na kuandika kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili,"alisema Msuva.

Naye Mhamasishaji Jamii kutoka Room to Read Rogathe Matulo amesema  kwamba katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora wamekuwa wakiwafundisha stadi za maisha ili kuwaongezea kujiamini.

Matulo amebainisha kwamba  wanawafundisha stadi za maisha ili wawe na maamuzi sahihi akiwa shuleni na aweze kupata elimu kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne na siyo kuishia njiani.

Shirika hilo la Room To Read linatekeza mradi huo wa kuwasaidia watoto wa kike katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam,Tanga pamoja na Mkoa wa Pwani inatekeleza katika shule nne zilizopo katika Halmashauri ya mji Kibaha.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...