Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Safi Tanzania (REA) wamezindua rasmi mradi mkubwa ambao utawafikia na kuwawezesha wafanyakazi wote wa Magereza kuacha matumizi ya mkaa na kuni na kuhamia matumizi ya gesi.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Julai 1,2025 katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu ambapo kupitia mradi huo Oryx Gas imewwzesha upatikanaji wa mitungi ya kg 15 na majiko ya sahani mbili pamoja na viunganishi vyake kwa punguzo kubwa ambapo REA wao wamewalipia askari na maofisa kwa niaba ya Serikali.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Meneja wa Miradi Safi ya Kupikia kutoka Oryx Gas Tanzania LTD Peter Ndomba amesema pia kampuni hiyo kwa kushirikiana na msambazaji wake mkuu wa mkoani Simiyu wametoa punguzo la kudumu kwa kila askari aliyenufaika na mradi huo.

“Mtungi wa gesi unapoisha atajaziwa tena kwa bei nafuu.Punguzo hilo la kujaza gesi litaendana na kupelekewa nyumbani mara gesi inapoisha.Ugawaji wa mitungi umeenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi salama ya gesi.

“Hii ni utekelezaji wa sera ya kampuni ya Oryx Gas ya kutoa mafunzo ya matumizi salama ya gesi kwa kila mtumiaji wa mtungi wa Oryx,siku zote tumekuwa tuhakikisha mtumiaji wa mtungi wa gesi ya Oryx anakuwa salama na katika hilo tumekuwa tukitoa elimu ya matumizi salama ya gesi na tutaendelea na utaratibu huu siku zote.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...