Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Innocent L. Bashungwa amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Karagwe, mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bashungwa amechukua fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Karagwe, Ndugu Anatory Nshange, leo tarehe 01 Julai 2025.

Bashungwa amekuwa mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa vipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 na 2020 hadi 2025, ambapo ameaminiwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama na Serikali ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo; Waziri wa Viwanda na Biashara; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Waziri wa Ujenzi; na kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...