Na Mwandishi wetu, Mbozi Songwe.
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-razaq Badru amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo waliopo kituo cha Kimondo cha Mbozi mkoani Songwe kufanya kazi kwa ari kubwa na kujituma ili eneo hilo liweze kuwa kitega uchumi muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kamishna Badru ametoa rai hiyo alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na watumishi wa kituo hicho na kusisitiza kuwa Serikali kupitia NCAA imefanya kazi kubwa ya kuboresha eneo hilo kwa kujenga jengo jipya la makumbusho ya kisasa na kuweka vioneshwa mbalimbali hasa vinavyohusu mila na desturi za makabila ya mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuvitangaza na kufanya eneo hilo kuwa kitega uchumi kizuri kwa maendeleo ya taifa.
Aliwaeleza watumishi hao kuwa uwepo wao katika kituo hicho ni muhimu kwa kuwa NCAA ina mipango ya kuboresha zaidi mazingira ya hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea na kufanya eneo hilo kuwa chanzo kizuri cha mapato kwa Serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Kimondo cha Mbozi Afisa Uhifadhi Mwandamizi Andrew Lowasa amemweleza kamishna wa Uhifadhi kuwa kituo hicho katika mwaka wa fedha 2024/2025 kimetembelewa na wageni 2,525 kutoka ndani na nje ya nchi
Kamishna wa Uhifadhi NCAA Abdul-razak Badru yupo kwenye ziara ya kuvitembelea vituo mbalimbali vya urithi wa utamaduni na Mambokale vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo nje ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kukagua utendaji kazi katika maeneo hayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...