Katika harakati za kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, jina la Ambrose Ambrose Komba, anayejulikana zaidi kwa jina la Majamuni, limeanza kuchukua nafasi ya kipekee katika mioyo ya wananchi wa Kata ya Amanimakolo, mara baada ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ngazi ya Udiwani na Ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi kukamilika.
Majamuni ametia nia ya kugombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Amanimakolo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Ni kijana mwenye umri wa miaka 36, mzaliwa na mkazi wa kijiji cha Amanimakolo, eneo ambalo awali lilikuwa sehemu ya Kata ya Kigonsera, baadaye likawa Mkako na sasa ni Kata kamili inayojitegemea.
Majamuni ni kiongozi mwenye historia halisi ya eneo analolitaka kulitumikia, Alikulia katika mazingira ya kawaida akielewa kwa undani changamoto zinazowakabili wananchi wa Amanimakolo. Alipata elimu ya Msingi shule ya msingi Amanimakolo, na elimu ya sekondari katika shule ya Nguruma, iliyopo kijiji cha Luhimba, Kata ya Mtyangimbole, Halmashauri ya Madaba, na kuhitimu mwaka 2007.
Baadaye alijiunga na chuo cha mafunzo ya elimu ya ufundi stadi yaani (VETA), ambako alijifunza ujuzi unaohusiana na maisha ya vitendo, jambo lililomjenga kuwa kijana wa kutenda zaidi kuliko kusema.
Dhamira yake ya kuwania nafasi ya udiwani inatokana na hali halisi ya maisha ya watu wa Amanimakolo, hasa vijana na wanawake, Majamuni anaamini kuwa vijana wengi wanakosa fursa kwa sababu ya ukosefu wa taarifa, mwamko mdogo na kutoshirikishwa katika maamuzi ya maendeleo.
Kupitia nafasi ya udiwani analenga kuwa daraja la kuunganisha vijana na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 kutoka mapato ya Halmashauri kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Kupitia mpango madhubuti wa uhamasishaji, uratibu wa vikundi, na usaidizi wa kiufundi katika uandishi wa miradi, Ambrose anataka kuhakikisha kila kijana mwenye ndoto Amanimakolo anapata fursa ya kujiendeleza kiuchumi bila kikwazo, anaamini kuwa uwezeshaji wa mtu mmoja mmoja, hasa katika kaya za kipato cha chini, ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli ya jamii nzima.
Mbali na ajenda ya vijana, Majamuni ameweka msisitizo mkubwa katika kuboresha huduma za jamii, ajenda yake inajumuisha uboreshaji wa miundombinu ya shule, ujenzi wa madarasa na madawati, kuboresha vituo vya afya, kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama, pamoja na kuunganisha vijiji kwa barabara zinazopitika kwa mwaka mzima.
Katika Kata ya Amanimakolo, migodi ya makaa ya mawe ni rasilimali muhimu ambayo bado haijawanufaisha wananchi kwa kiwango kinachotarajiwa, Majamuni ana mpango wa kusimamia kwa karibu mashirikiano kati ya wawekezaji wa migodi na jamii inayowazunguka ili mapato ya rasilimali hizo yachangie moja kwa moja maendeleo ya jamii kwa njia ya uwazi na uwajibikaji.
Licha ya kujikita kwenye maendeleo ya miundombinu na uchumi, Majamuni pia anasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika kila hatua ya maendeleo, anaamini kuwa maendeleo ya kudumu hayawezi kufikiwa bila kushirikiana na wananchi katika kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi yote ya kijamii.
Majamuni ni mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu mwaka 2004, akiwa na historia ya kuwa mstari wa mbele katika shughuli za chama, anajitambulisha kama kijana wa itikadi, lakini zaidi ya hapo, ni kiongozi wa watu, Udiwani kwake si heshima binafsi, bali ni wito wa kutoa huduma kwa uadilifu na kujituma.
Kwa kifupi, Ambrose Komba maarufu kwa jina la Majamuni ni chaguo la kizazi kipya kijana mwenye maono, msimamo, na uwezo wa kutatua changamoto za kweli kwa njia halisi, dhamira yake ni kuhakikisha Kata ya Amanimakolo inakuwa mfano wa maendeleo shirikishi, endelevu na yanayogusa maisha ya kila mwananchi kuanzia ngazi ya kaya, wananchi wa Amanimakolo muungeni mkono katika harakati zake za kutaka kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...