NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wamesaini mkataba wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe.

Mradi huo ambao utatekeleza katika mkoa wa Geita utasaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji na upatikanaji wa mkaa mbadala ili kuboresha uchumi kwa kuongeza ajira, kipato kwa wananchi na serikali pamoja kuongeza soko la matumizi ya mkaa mbadala na kulinda mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti.

Katika mkataba huo, REA itatoa jumla ya shilingi bilioni tatu (3,000,000,000) wakati STAMICO itachangia shilingi bilioni 1, 580, 000, 000 kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Katika mgawanyo huo, REA itagharamia ununuzi wa mtambo wakati STAMICO italipia upatikanaji wa kiwanja, ujenzi wa jengo la kiwanda na gharama za ufungaji wa mitambo.

Akizungumza leo Julai 22, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema mkataba huo utaenda kuongeza kasi ya upatikanaji wa mkaa mbadala na kwa bei nafuu ikiwa ni moja wapo ya lengo la mkakati wa nishati safi ya kupikia.

"Tunatambua kuwa utunzaji wa mtambo huu ni muhimu sana ili huduma iliyokusudiwa iendelee kutolewa kwa wakati bila kuathiri uchumi wa wananchi, afya pamoja na mazingira kwa ujumla". Amesema Mhandisi Saidy.

Aidha ameongeza kuwa Wakala unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha mkakati wa nishati safi ya kupikia unatimiza malengo yaliyowekwa.

Amesema Wakala utaendelea kushirikiana na STAMICO kuongeza mitambo mingine zaidi katika maeneo mbalimbali nchini kulingana na upatikanaji wa fedha.

Pamoja na hayo Mhandisi Saidy amesema kuwa Wakala unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo usambazaji wa majiko banifu, usambazaji wa majiko ya umeme, LPG za kilo 6 na 15, usambazaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Pwani pamoja na ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika taasisi za Umma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse amesema ushirikiano huo utasaidia Shirika kutimiza ndoto yake ya kuhakikisha wananchi wote wanaachana na nishati chafu ya kupikia ifikapo mwaka 2034, hivyo kuunga juhudi za Serikali za kutunza mazingira.

"Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wake ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kumkomboa mwanamke ili aachane na nishati chafu, hivyo STAMICO tumejipanga kutekeleza maono haya ya kiongozi wetu". Amesema Dkt. Mwasse.

Hata hivyo Dkt. Mwasse ameongeza kuwa nishati ya Rafiki Briquettes kwa sasa inatumiwa na taasisi nyeti kama vile Jeshi la Magereza ambapo Magereza yote 129 kote nchini yanatumia nishati hii kama aina mojawapo ya nishati ya kupikia, vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Nyingine taasisi za elimu kama vile vyuo, shule za msingi na sekondari, hoteli, mgahawa, wachoma nyama na chips.

Amesema kuwa STAMICO itaendelea kutunza mitambo hiyo ili iendelee kutoa huduma inayostahili.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam




Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi (kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kulia) mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam



Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kulia) wakionesha mikataba waliosaini ya makubaliano wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano na STAMICO kwaajili ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano na REA kwaajili ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano wa ushirikiano wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala unaotambulika kwa jina la Rafiki Briquettes unaotokana na vumbi la makaa ya mawe. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 22, 2025 katika ofisi wa REA Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...