Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) Prof.Mkumbukwa Madundo Mtambo amepongeza maandalizi na uboreshaji uliofanywa ndani ya Maonesho hayo yanayoendelea ndani ya Uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba).

Prof Mtambo alitembelea mabanda kadhaa kabla ya kufika katika banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo TIRDO pia ni washiriki .

Katika Maonesho hayo ,Prof.Mtambo alieleza kuwa katika Maonesho haya ,TIRDO inashikiri ikiwa na wataalam kutoka idara mbali mbali lakini zaidi ni katika kuonesha ubobevu katika Idara za Nishati ,Mazingira ,Kemia ya Viwanda na pia kutambulisha Maabara ya Chakula ambayo imepata ithibati ya kufanya upimaji wa aina mbali mbali ya vyakula .

Prof.Mtambo pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza watumishi wake wanaoshiriki katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...