NA Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego ameeeleza kuwa wastani wa patoa la Mwananchi mmoja mmoja Mkoani humo umeongezeka kutoka Shilingi Milioni 1,588,604.66 kwa mwaka 2020/21 hadi kufikia Shilingi Milioni 1,710,562.00 mwaka 2024/25.
Ambayo ni sambamba na ongezeko la Pato la Mkoa huo ambalo limeongezeka kutoka Trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi kufikia Trilioni 3.398 mwaka 2024/25.
Mhe Dendego ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma akielezea Mafanikio ya Mkoa wake katika kipindi miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, leo Julai 4,2025.
Ambapo amesema pamoja na hayo pia kumekuwa na maongezeko ya Makusanyo ya Ndani na yale ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)ambayo yamefikia Bilioni 30 mwaka 2024/25 kutoka Bilioni 11.9 mwaka 2021/22 na Makudanyo yale ya Ndani kufikia Bilioni 24.8 mwaka 2024/25 kutoka Bilioni 14.6 mwaka 2020/21.
"Pato la Mkoa limeongezeka kutoka Trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi Shilingi Trilioni 3.398 kwa mwaka 2024/25,pamoja na wastani wa pato la Mwananchi mmoja mmoja kuongeza kutoka Shilingi 1,588,604.66 mwaka 2020/21 hadi Shilingi 1,710,562.00 mwaka 2024/25".
"Pia makusanyo ya TRA yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 11.9 mwaka 2021/22 hadi Shilingi Bilioni 30 mwaka 2024/25 ikiwa ni sawa na asilimia 152,huku makusanyo ya mapato ya Ndani yakiwa yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 14.6 2020/21 hadi Shilingi Bilioni 24.8 mwaka 2024/5 ikiwa ni sawa na asilimia 69.8".
Aidha akizungumzia shughuli za kiuchumi na uzalishaji amesema Mkoa umeendelea kujitosheleza kwa chakula ambapo uzalishaji umeongezeka toka wastani wa tani 649,850 hadi tani 1,325,201 kwa mwaka.
Mkoa wa Singida umegawanyika katika Wilaya 5, na kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Mkoa una idadi ya wakazi wapatao 2,008,058 ambapo wanaume ni 995,703 na wanawake ni 1,012,355, ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita jumla ya watu 637,421 sawa na asilimia 3.8 wameongezeka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...