Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo Bi. Mwanahiba Mzee, akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo Bi. Mwanahiba Mzee, akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Taasisi hiyo, kufahamu fursa zitolewazo na Taasisi hiyo.
Afisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko wa Pembejeo, Mhandisi, Manolana Aloyce, (wa pili kulia), akisisitiza jambo, alipokuwa akizungumza na mwananchi aliyetembelea katika Banda la Mfuko huo, Maonesho ya 49 ya Sabasaba, Jijini Dar es laam.
Afisa Uendeshaji, Mfuko wa pembejeo Bw. Ally Wajihi, (wa kwanza kulia), akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda hilo, kwenye naonesho ya Sabasaba, Dar es Salaam.
Na: Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Katika kuhakikisha wananchi wanaojihusisha na kilimo wanapata fursa za mikopo kuendeleza shughuli zao, Mfuko wa Pembejeo AGITF, umeendelea kujiimarisha kwa kuhakikisha kwamba wadau hao muhimu wanapata fursa hiyo muhimu, ikiwamulika zaidi wakulima wadogo na wa kati, wenye ekari zisizozidi 50, na wale anaowanufaisha wakulima wenzie
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayofanyika Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bi. Mwanahiba Mzee, amesema kuwa Mikopo wanayoitoa ni ya masharti nafuu na riba nafuu ambayo ni rafiki kwa wanachi wa kawaida.
"Maeneo ambayo tunatoa fedha za mikopo ni kuanzia shambani kwa maana kuanzia mtu anapoandaa shamba lake, pembejeo zote za kilimo, miundombinu ya umwagiliaji mpaka wakati anavuna, lakini pia tunatoa zana za kilimo kama power tiller" amesema.
Aidha, amesema kuwa, aina ya mikopo nafuu inayotolewa na Mfuko huo inawalenga vijana na wanawake, kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupata mitaji na uzoefu, kwani wengi wao hawamiliki dhamana za kupata mikopo hiyo.
Ameongeza kuwa, kwenye uchakataji wa mazao, wanatoa mashine mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile zinazotumika kuchakata mafuta, mchele, uzalishaji wa unga na mvinyo, nakwamba Mfuko huo unawalenga hasa wakulima ambao wakienda kwenye taasisi za fedha wanakosa vigezo vya kupata mikopo kutokana na wengi wao kukosa hati itakayomuwezesha kupata mikopo hiyo.
"Kwa wanawake na vijana tuna aina mkopo unaoitwa Mkulima Nafuu, ambayo tunakopesha kwa asilimia 4.5 kwa mwaka kwa vijana kuanzia miaka 18 hadi 40 kwa wanaume, na wanawake hadi umri wa miaka 65 na dhamana sio kipaumbele" ameongeza.
Mfuko wa Pembejeo unatimiza miaka 30 mwaka huu tangu kuanzishwa kwake, ambapo katika kipindi chote umekuwa kimbilio kwa wananchi mbalimbali na kuweza kukopesha jumla ya Bilioni 95 kwa wakulima wadogo, pamoja na pembejeo yakiwemo matrekta zaidi ya 1,500, na kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula nchini, pamoja na kuongeza ajira kwa vijana wengi nchini nzima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...