Benki ya Exim Tanzania Yazindua Elite Banking

Dar es Salaam: Katika hatua ya kihistoria ya kuendeleza ahadi yake ya kuwapa wateja wake huduma bora, Exim Bank imebadilisha maana ya huduma za kibenki za kipekee kwa kuzindua rasmi huduma yake ya ‘Elite Banking’. Uzinduzi huu ulifanyika katika hafla iliyohudhuriwa na watu maalum katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wateja mashuhuri, wajumbe wa bodi, na washirika wa benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu, alitoa shukrani za dhati kwa wateja wao ambao wamekuwa nguzo ya mafanikio ya benki hiyo kwa miaka mingi. "Elite Banking si huduma mpya tu, bali ni ishara ya dhamira yetu ya kuwaweka wateja wetu wa thamani katika kila tunachokifanya," alisema Matundu.

Lengo la uzinduzi huu ni 'Kutafsiri Upya Dhana ya Upekee'. Hii inaashiria mabadiliko kutoka kwenye dhana ya zamani ya kipekee inayotegemea hadhi, kwenda kwenye mtazamo wa kisasa unaozingatia umuhimu, kubinafsisha huduma, na kutoa fursa zenye hadhi. Matundu aliongeza, "Upekee huu mpya unahusu zaidi ya bidhaa za kipekee. Unaakisi dhamira yetu ya kutoa uzoefu wa kibinafsi, huduma maalum za kipekee, na huduma inayoweza kutambua mahitaji ya mteja na hata kuvuka matarajio yake."

Kwa upande wake, Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja katika Benki ya Exim Tanzania, alifafanua zaidi kuhusu huduma ya ‘Elite Banking’ na kutambulisha timu maalum ya usimamizi wa mahusiano ya wateja. Alisema kuwa huduma hii ni suluhisho kwa ajili ya mahitaji ya wateja wenye hadhi ya juu kwa kutoa urahisi na huduma iliyoboreshwa.

“Elite Banking imeundwa kuwasogezea wateja wetu ulimwengu wa huduma za kidigitali karibu zaidi popote walipo - kuanzia maeneo maalum ya kusubiria kwenye matawi yetu, huduma za kimataifa kwenye viwanja vya ndege kupitia Mastercard DragonPass, hadi suluhisho za kifedha zilizoboreshwa na faida za kipekee popote walipo na wakati wowote,” alifafanua Lyimo.

Uzinduzi huu unajengwa juu ya msingi imara uliowekwa na huduma ya ‘Preferred Banking’ iliyoanzishwa mwaka 2016, na sasa unavuka mipaka kwa kutoa suluhisho za kibenki za kipekee kwa haraka na kwa ubora zaidi.

Kilele cha hafla hiyo ilikuwa ni uzinduzi wa huduma za Kadi za Mastercard World, zilizoundwa kwa ushirikiano na Mastercard. Huduma hii inajumuisha kadi tatu za hadhi ya juu: Mastercard World Debit Card (TZS), Mastercard World Debit Card (USD), na Mastercard World Credit Card.

Kadi hizi za kifahari zinafungua ulimwengu wa faida zisizo na kifani, zikiwapa wateja wa ‘Elite Banking’ fursa za kupata maeneo maalum ya kusubiria kwenye viwanja vya ndege kote duniani, huduma maalum za kipekee na huduma za usafiri wa kifahari, pamoja na bima kamili ya kusafiri inayojumuisha kila kitu kuanzia ajali hadi matibabu ya dharura. Wamiliki wa kadi hizi pia wanapata ulinzi thabiti wa manunuzi duniani kote, pamoja na zawadi za kipekee kwa ajili ya manunuzi, milo, usafiri, na burudani, zote zikiendeshwa na teknolojia ya kisasa ya malipo isiyotumia fedha taslimu.

Elsie Wachira-Kaguru, mwakilishi wa Mastercard - Tanzania, Burundi na Djibouti, alielezea kufurahishwa na ushirikiano huu. “Mastercard tuna furaha kuzindua huduma hizi mpya za kadi kwa kushirikiana na Exim Bank Tanzania, kufungua ulimwengu wa fursa za kipekee kwa wateja, huku tukilenga kuunda suluhisho zisizo na kifani. Tunajivunia kuendeleza mabadiliko ya kidijitali katika mfumo wa malipo nchini Tanzania kupitia ushirikiano wenye manufaa kama huu,” alisema.

Pamoja na mapinduzi ya huduma bora na za kisasa, ‘Elite Banking’ inafungua ukurasa mpya wa huduma zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa kidijitali. Benki ya Exim Tanzania inabadilisha maana ya upekee kuwa jambo lenye mashiko, ikitoa suluhisho zilizojengwa juu ya uaminifu na teknolojia ili kuwawezesha wateja wake kufikia malengo yao makubwa na mapana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank Tanzania, Bw. Jaffari Matundu, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya ‘Elite Banking’, huduma inayoleta mapinduzi mapya katika sekta ya fedha. ‘Elite Banking’ imejengwa katika msingi mmoja wenye nguvu: Maana Mpya ya Huduma za Kipekee. Huduma hii inawapa wateja wake ulimwengu wa fursa, ikiwemo maeneo maalum ya kusubiria kwenye matawi, huduma za kimataifa kwenye viwanja vya ndege kupitia Mastercard DragonPass, na matumizi ya huduma za kadi za Mastercard World, yote yakiendeshwa na timu maalum ya usimamizi wa mahusiano ya wateja. Hafla hii ya uzinduzi ilifanyika tarehe 30 Julai 2025, jijini Dar es Salaam.

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...