Kampuni inayoongoza barani Afrika katika huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni, Bolt, imetoa taarifa kuwa nchini Tanzania, madereva wake 50 wanaoongoza—ambao wengi wao ni wa kundi la magari—wameweza kutengeneza wastani wa shilingi milioni 21,903,460 (TSh) za mapato halisi katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hii inamaanisha kuwa kila dereva alipata wastani wa shilingi 3,650,577 kwa mwezi.
Takwimu hizi zinaonesha kwa dhahiri nafasi ya kipekee ambayo gig economy (ajira zisizo za kudumu lakini zenye tija kupitia majukwaa ya kidijitali) inachukua katika soko la ajira la Tanzania. Kiasi hicho pia kimewapiku hata mameneja wa sekta rasmi, jambo linaloibua mjadala kuhusu usawa wa malipo na mustakabali wa ajira nchini.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mshahara wa wastani katika sekta rasmi mwaka 2023/24 ulikuwa TSh 609,354 kwa mwezi—ikiwa ni TSh 549,373 katika sekta binafsi na TSh 1.27 milioni katika sekta ya umma. Katika muktadha huu, mafanikio ya madereva wa Bolt si jambo la bahati nasibu; yanaibua mtazamo mpya kuhusu tija na malipo katika ajira zisizo za kawaida.
Kihistoria, muktadha wa kiuchumi pia unatoa picha pana ya mabadiliko haya. Uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, huku makadirio ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) yakitabiri ukuaji kufikia asilimia 6 mwaka 2025. Hata hivyo, changamoto za ajira bado ni kubwa, kwani Shirika la Kazi Duniani (ILO) linakadiria ukosefu wa ajira kufikia asilimia 8.9 mwaka 2023. Ingawa kazi ya udereva wa huduma za mtandaoni haijawahi kuchukuliwa kama taaluma yenye heshima, hali hii inaonyesha kuwa sasa imekuwa chaguo halisi linalowawezesha wanaume na wanawake kujipatia uhuru wa kifedha.
Sekta ya usafiri, kwa upande mwingine, inaendelea kuonesha nafasi na changamoto. Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam umeongeza ufanisi wa usafiri wa umma, lakini bado unakabiliwa na mapungufu katika upatikanaji na huduma za umbali mfupi (first/last-mile), kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia – Tanzania Urban Transport Review. Wakati huo huo, mabadiliko ya bei za mafuta duniani na kuyumba kwa thamani ya fedha yameendelea kuwa changamoto ya kimuundo kwa madereva na abiria, licha ya hatua za serikali kudhibiti bei.
Akizungumzia matokeo haya, Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania, alisema: “Takwimu hizi za mapato zinaonyesha zaidi ya simulizi za mafanikio ya mtu mmoja mmoja—zinaashiria jinsi majukwaa ya kidijitali yanavyounda maeneo yenye tija kubwa yanayoweza kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza kipato cha kaya. Tumejipanga kuendelea kutoa fursa zaidi kwa madereva wetu. Ushirikiano wao thabiti kwenye jukwaa unaweza kuzaa matokeo makubwa ya kifedha. Mkazo wetu ni kuboresha uzoefu wa madereva na kuhakikisha uendelevu wa ajira katika gig economy.”
Bolt inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuboresha ustawi wa madereva, ikiwemo vipengele vya usalama, muda wa kazi unaonyumbulika, pamoja na motisha. Katika kiwango cha kitaifa, changamoto iliyo mbele ni kuandaa mazingira wezeshi ya kisera na kiuchumi yatakayopanua fursa hizi za kipato, si kwa wachache tu wanaoongoza bali kwa idadi kubwa ya watanzania, na hivyo kuchangia mageuzi jumuishi katika soko la ajira.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...