Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma M. Abdallah, aliwasilisha mada kwa Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi za Umma.
Katika wasilisho lake, Bi. Abdallah aliwataka SOEs kuachana na urasimu na kuzingatia mbinu bunifu za kisasa ambazo zitarahisisha taratibu za kiutendaji na kuharakisha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Alisisitiza pia umuhimu wa kuanzisha mfumo thabiti unaojengwa juu ya utawala bora, uwazi,matumizi sahihi ya data, biashara endelevu na viashiria vya utendaji (KPIs) ili kuongeza tija na kuboresha matokeo ya huduma.
Kwa upande wake, Puma Energy Tanzania inajivunia mafanikio chanya yaliyopatikana kupitia mfumo wa nguzo tano unaojikita kwenye: Uongozi thabiti, Mageuzi ya sera, Miundombinu ya kidijitali, Nguvu kazi yenye wepesi na Utamaduni wa utendaji unaoendeshwa na matokeo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...