Na Mwandishi wetu, TADB
Upatikanaji wa huduma za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) visiwani Zanzibar umefungua fursa mpya za kiuchumi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kupitia mikopo nafuu, elimu ya fedha na uhusiano wa moja kwa moja na masoko ya uhakika.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TADB Kanda ya Zanzibar leo Agosti 5, 2025 katika maeonesho ya NaneNane Kitaifa jijini Dodoma wakati wa mahojiano maalumu kuhusu utekelezaji wa Benki hiyo kwa upande wa Zanzibar.
"TADB imewezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kisasa, uvuvi endelevu, usindikaji wa mazao ya kilimo, biashara ndogondogo zinazoendeshwa na vijana na wanawake kwenye mnyororo wa thamani ya Sekta za kilimo, mifugo na uvuvi", alisisitiza Singoi
"Hadi sasa jumla ya miradi 43 imenufaika moja kwa moja na huduma hizi, ikiwemo miradi 7 inayomilikiwa na wanawake na miradi 4 ikiwa ni vijana . Sanjari na hayo jumla ya miradi10 imefadhiriwa ikiwa inamilikiwa na vyama vya ushirika (8 kutoka Pemba na 2 kutoka Unguja). Miradi yote hii imeunganishwa katika mifumo rasmi ya kibenki na masoko," alisisitiza Singoi
TADB Kanda Zanzibar imewezesha miradi inayohusisha uzalishaji wa mazao ya biashara kama karafuu, ufugaji wa kuku wa mayai, uvuvi wa samaki kwa vizimba, pamoja na kilimo mseto kinachowahusisha vijana na wanawake. Aidha, benki imekuwa ikitoa mafunzo ya kilimo biashara na ujasiriamali kwa wakulima wapya jambo lililowasaidia kubadili mtazamo kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo chenye tija.
Mpaka sasa kwa mijibu wa Singoi zaidi ya zaidi ya wanufaika 200 wameshafikiwa kupitia mradi huu ambapo jumla ya ng’ombe wa maziwa (Improved heifers) 352 wenye thamani ya shilingi 993,294,050 wametolewa vilevile wafugaji hao waliopatiwa mikopo wamepewa ruzuku fungamanifu zenye thamani ya TZS 222,000,000 ili kuwapunguzia mzigo wa ulipaji mikopo ili kuongeza tija na uzalishaji.
Pia, kwa kushirikiana na Idara ya Mifugo Zanzibar na Shirika la Heifer International, Mradi huu pia umewezesha elimu ya ufugaji bora, uhimilishaji wa kisasa, upatikanaji wa mbegu bora za mifugo, lishe bora, na uwezeshaji wa vifaa kama pikipiki za maafisa ugani, mashine za kukatia majani, vifaa vya tiba, kompyuta na miundombinu ya ukusanyaji maziwa, jumla ya wafugaji 1583 (wanawake 453) wamefikiwa.
Mipango ya sasa inahusisha uwezeshaji wa miradi ya kilimo cha baharini kama vile ufugaji wa majongoo bahari, na usindikaji wa mazao ya kilimo unaofanywa na wanawake na vijana.
Benki imeidhinisha fedha kiasi cha bilioni 22 kwa ajili ya mwaka huu wa 2025, bilioni 16 zikienda kwenye karafuu, bilioni 3.8 zikienda kwenye wafugaji wa kuku, wafugaji wa ng’ombe wa maziwa bilioni 1.1 , wakulima wa mboga mboga 1.2.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...