*Aweka wazi mikakati wa kuifungua Pangani kwa miundombinu ya barabara
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Pangani
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi mbalimbali ambazo Serikali inakwenda kuyatekeleza katika miaka mitano ijayo katika Wilaya ya Pangani mkoani Tanga huku akitumia nafasi hiyo kuzungumza Ujenzi wa barabara ya Bagamoyo-Saadan-Pangani hadi Tanga ambayo unaokwenda adha ya usafiri.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Pangani katika mkutano wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu Dk. Samia amesema Februari mwaka huu alifika Pangani kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Mto Pangani na barabara ya Bagamoyo - Saadani - Pangani - Tanga.
Amesema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakisubiri barabara hiyo ambayo itawaondolea adha ya kulazimika kusafiri masafa marefu kwa kukosa muunganiko kati ya wilaya za Bagamoyo na Pangani.
"Barabara hii inaendelea vizuri na itakwenda kufungua ukanda wa Pwani kiuchumi na kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji.
"Kwa wale ambao hawajapata fursa ya kusoma Ilani naomba nigusie kwamba tunapoanza na barabara hii kwa kipande cha Tanga - Pangani kilometa 50 ujenzi umefikia asilimia 75," amesema
Ameongeza kipande cha Pangani - Saadani - Makurunge chenye kilometa 95 ujenzi umefikia asilimia 50 huku daraja la Mto Pangani lenye mita 525 na barabara unganishi imefikia asilimia 60.
Akieleza mbele ya wananchi hao Dk. Samia amesema ahadi ya CCM kwa wananchi wa Pangani ni kuikamilisha barabara hiyo ambapo siyo muda mrefu wananchi wataanza kufaidi matunda.
Kuhusu uvuvi Dk.Samia amesema Serikali imewezesha upatikanaji boti 15 zinazosafiri kwa umbari mrefu baharini kwa shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki.
"Ninakumbuka nilizindua mradi huu wenye thamani ya Sh. bilioni 1.6 ambao utaongeza fursa za ajira kwa vijana wetu. Sambamba na hilo tumeanza ujenzi wa soko la samaki la kimataifa Kata ya Kipumbwi.”
Amefafanua mradi huo wa sh. bilioni 1.3 utakuwa na vifaa vya kukaushia dagaa ni muhimu katika kuwaongezea kipato wavuvi na kuchochea maendeleo ya wilaya yetu.
Ameongeza katika awamu ijayo serikali kali yake itaendelea kuwashika mkono wavuvi ili kuongeza vipato vyao.
Akizungumza kuhusu wafugaji, amesema kwamba serikali itaendelea kuleta mageuzi sekta ya ufugaji kuwa ya kisasa.
“Kwa Pangani serikali imetoa ng'ombe wa maziwa 51 huku kitaifa ikitoa ruzuku ya chanjo bure kwa kuku na nusu bei kwa mifugo mingine."Hii tumeifanya kupandisha thamani ya mifugo yetu. Tumehangaika kwa muda mrefu kutafuta masoko ya kimataifa. Tumepata masoko makubwa.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...