Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi mapema leo Oktoba 20, 2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kilwa mkoani Lindi,ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Ikiwa zimebaki siku 9 za lala salama kufikia uchaguzi mkuu,Dkt. Nchimbi anatarajia kufanya mkutano wake wa hadhara wa kampeni wa kunadi Sera na Ilani ya CCM (2025-2030) katika kata ya Tingi, jimbo la Kilwa Kaskazini na kuomba ridhaa ya wananchi kukipigia kura za ndio chama hicho kupitia wagombea wake katika nafasi zote kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025..jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...