Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndugu Kailima Ramadhani amejitokeza leo tarehe 29 Oktoba, 2025 kupiga kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Chaduru, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mkoani Dodoma.
Baada ya kupiga kura alifanya ziara ya kuvikagua vituo vya kupiga kura vya Shule ya Msingi Kisasa, Chaduru na Kituo cha Chilewa kilichopo katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Chilewa, Chang'ombe, jijini Dodoma.
Watanzanzia kote nchini leo wanapiga kura kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara.
Uchaguzi huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo "Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura" ambapo vituo vimefunguliwa saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.

















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...