Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahimiza wananchi kuendelea kujitokeza katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki zoezi la kupiga kura ya kuchagua Rais, Mbunge na Diwani akiwa katika Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 29 Oktoba 2025. Amewahimiza wananchi kutumia haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura kwa amani na utulivu.
Pia amewashukuru wanakijiji wa Kasumo kwa kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kuchagua viongozi.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...