Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Kilimo na Viwanda TCCIA mkoa wa Ruvuma Gideon Mpilime, amesema kuwa mshikamano na mipango madhubuti ya TANESCO ni nguzo muhimu zitakazosaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma katika kuwahudumia wateja kwa ufanisi, ametoa wito kwa viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanapanga kwa nia ya dhati ili kufanikisha malengo ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoandaliwa na TANESCO mkoani humo, Mpilime alieleza kuwa shirika hilo lina jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya nishati ya umeme, ameeleza kuwa kwa sasa TANESCO inamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na mazingira.

Mpilime amesisitiza kuwa sasa kuna vifaa vya umeme vya kupikia visivyotumia umeme mwingi, hivyo ni muhimu wananchi wakapatiwa elimu juu ya matumizi yake ili kuachana na matumizi ya kuni na mkaa vinavyoathiri afya na mazingira, ameongeza kuwa matumizi ya umeme kama nishati ya kupikia yatasaidia kuwaondolea kinamama changamoto mbalimbali za kiafya walizokuwa wakikumbana nazo hapo awali.

Aidha ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Ruvuma imeimarika kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma, amesema kuwa kukatika kwa umeme kumepungua na wateja sasa wanafurahia huduma bora, hali ambayo ni matokeo ya uongozi thabiti ndani ya TANESCO.8

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu huduma za umeme yamepungua kwa kiwango kikubwa, na akatoa pongezi kwa TANESCO kwa kuendelea kuboresha miundombinu na huduma kwa wateja, amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni uthibitisho wa uwepo wa usimamizi mzuri na jitihada za dhati za shirika hilo.

Hafla hiyo ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ilifanyika leo Oktoba 10, na ilihudhuriwa na wafanyakazi wa TANESCO pamoja na wadau mbalimbali kutoka Chemba ya Biashara, Kilimo na Viwanda mkoani Ruvuma, Wadau hao walitumia fursa hiyo kuzungumzia namna bora ya kushirikiana katika kuboresha huduma za umeme kwa  maendeleo ya mkoa huo pamoja na kupokea zawadi mbalimbali kutoka TANESCO.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...