MKOA wa Ruvuma, katika msimu wa mauzo ya zao la korosho 2025/2026, umepanga kukusanya zaidi ya tani 35,000 sawa na kilo 35,000,000, ikiwa ni ongezeko la kilo 3,391,962 zilizouzwa katika msimu wa kilimo 2024/2025.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amesema hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, kwenye mkutano wa wadau wa zao la korosho uliofanyika mjini Tunduru.
Brigedia Abbas alisema takwimu za uzalishaji wa korosho zinaongezeka mwaka hadi mwaka, kwani katika msimu wa 2024/2025 mkoa huo ulizalisha kilo 31,608,038 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 93.14, ikiwa ni ongezeko la kilo 5,545,715 sawa na asilimia 58.38.
“Katika msimu wa 2023/2024 wakulima wa mkoa huo walifanikiwa kuzalisha jumla ya kilo 26,062,323 zenye thamani ya shilingi bilioni 45.5, huku bei ikiwa kati ya shilingi 2,947 hadi 3,510 kwa kilo moja,” alisema Abbas.
Alisema zao la korosho ni kati ya mazao makuu ya kilimo katika mkoa wa Ruvuma lenye mchango mkubwa kimaendeleo na kiuchumi kwa mkoa, taifa na kwa mkulima mmoja mmoja, ambapo wakulima wengi wamefanikiwa kuboresha maisha yao na kujiletea maendeleo kupitia zao hilo.
Aidha, alisema Serikali imetoa kwa wakulima wa korosho viuatilifu bure na mabomba ya kupulizia kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuwapunguzia mzigo mkubwa wa kuhudumia mikorosho yao ili kuongeza tija.
“Wakulima wamenufaika na utaratibu wa upatikanaji wa pembejeo za korosho, ambapo kilo 5,962,550 za salfa ya unga zimesambazwa, viuatilifu vya maji lita 270,573 na sumu ya kudhibiti wadudu lita 110,432. Zoezi la upokeaji lilianza mwezi Aprili 2024 na kumalizika mwezi Septemba 2025,” alisema Abbas.
Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (TAMCU LTD), Marcelino Mrope, alisema uzalishaji wa zao la korosho katika mkoa huo unaongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na wadau wote kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya zao hilo, hasa upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za ugani.
Alisema kuanzishwa na kusimamiwa kikamilifu kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kumewezesha wakulima kuuza mazao yao kwa bei kubwa, ambapo msimu uliopita bei ya korosho ilikuwa shilingi 2,942.75 kwa kilo moja.
Aliongeza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika msimu wa 2024/2025 yametokana na maboresho ya sheria, kanuni na miongozo ya utekelezaji wa mfumo wa mauzo wa stakabadhi ghalani kwenye zao hilo.
Mrope ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kuongezeka kwa uzalishaji wa korosho ghafi, kuongezeka kwa ubora wa korosho ambapo korosho zote zilizozalishwa katika msimu huo zilikuwa daraja la pili.
“Mheshimiwa mgeni rasmi, mafanikio mengine ni kuongezeka kwa wakulima wanaofungua akaunti za benki kwa ajili ya kupokea malipo, kwani zaidi ya asilimia 98.5 wamefungua akaunti. Hivyo malipo yao hufanyika kwa wakati na wanalipwa ndani ya siku saba za kazi baada ya kufanyika kwa mnada,” alisema Mrope.
Alisema maandalizi ya msimu mpya huenda sambamba na vitendea kazi ikiwa ni pamoja na vifungashio, kamba, rangi, mizani, usafirishaji na maghala ya kuhifadhi korosho.
Aliongeza kuwa TAMCU, kwa kushirikiana na vyama vikuu vingine vinavyosimamia ukusanyaji wa zao la korosho, wameunda kampuni ya pamoja (KCJE LTD) inayoratibu na kusimamia upatikanaji wa magunia, ambapo wanahitaji magunia 437,500 na tayari wamepata magunia 600,000 yenye uwezo wa kuhifadhi korosho kilo 48,000,000.
Alisema usambazaji wa magunia kwa vyama vya ushirika vya msingi ulianza tarehe 23 Oktoba 2025 na unafanyika kwa awamu kutokana na uzalishaji wa korosho. Katika awamu ya kwanza, tayari wamesambaza magunia 250,000 kwa Amcos 43 kati ya 53 zilizopo mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani ya Njombe na Mbeya.
Mwenyekiti wa TAMCU, Mussa Manjaule, ameipongeza vyama vya msingi vya ushirika (Amcos) kwa kusimamia zoezi la ukusanyaji wa korosho katika msimu wa kilimo 2024/2025 licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...