Kisukari kinaendelea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa za kiafya zinazokua kwa kasi nchini Tanzania, na kuathiri maelfu ya watu kila mwaka, wengi wao bila kujua hali zao. Kuchelewa kutambua hali za afya zao, uelewa mdogo, pamoja na mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usio-faa, kutofanya mazoezi, na msongo wa mawazo, vimeendelea kuchochea ongezeko la ugonjwa huu, hasa kwa watu wanaofanya kazi, na kusababisha matatizo makubwa kama figo kushindwa kufanya kazi sawa sawa, kupoteza uwezo wa kuona, na hata vifo.

Kwa Kutambua ukubwa wa changamoto hii, Benki ya Exim imechukua hatua madhubuti ya kuunga mkono utambuzi wa mapema na kuhamasisha maisha yenye afya kwa jamii. Benki imeshirikiana na Chama cha Kisukari Tanzania (Tanzania Diabetes Association - TDA) kuunga mkono shughuli za kitaifa za Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2025, ikiwa ni ishara ya dhamira yake ya kuchangia kikamilifu katika jitihada za afya ya jamii, nje ya huduma zake za kifedha.

Kwa kuonesha msisitizo wa kuboresha ustawi wa jamii na wafanyakazi katika maeneo ya kazi kwa ujumla, Benki ya Exim imefanya zoezi la upimaji wa kisukari bure kwa wafanyakazi na wateja wake. Zoezi hili limeandaliwa kwa ushirikiano na Chama cha Kisukari Tanzania, ambacho kina utaalamu katika elimu, kinga na usimamizi wa ugonjwa wa kisukari.

Mpango huu unaendana na kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka huu, “Kisukari na Ustawi Mahali pa Kazi,” inayosisitiza umuhimu wa kutambua mapema, huduma za kinga na mitindo bora ya maisha ili kupunguza hatari za kuendelea kupata ugonjwa huu. Kwa kuleta huduma hii moja kwa moja kwa wafanyakazi na wateja, Benki ya Exim imewapa wateja na wafanya kazi wao fursa ya kujua hali zao za kiafya, kutambua viashiria mapema, na kuchukua hatua za kujilinda au kujua namna ya kusismamia ugonjwa huo ikiwa umegundundulika kuwa umeathirika.

Uchunguzi ulijumuisha vipimo mbalimbali vikiwemo:

• Tathmini ya mtindo wa maisha (mlo, unywaji pombe, uvutaji sigara, na kiwango cha mazoezi)

• Kipimo cha BMI, uzito na urefu

• Ufuatiliaji wa shinikizo la damu

• Kipimo cha sukari mwilini kwa kutumia glucometer

Kupitia vipimo hivyo, washiriki walipata kujua hali zao za sasa za kiafya na ushauri wa hatua za kuchukua ili kupunguza hatari ya kupata kisukari au kusimamia ugonjwa huo, endapo tayari umebainika.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu, alisema

“Wafanyakazi na wateja wetu ndio kiini cha kila tunachofanya. Afya ni msingi muhimu wa ustawi na tija. Kwa kutoa vipimo hivi, tunalenga kuwapa wafanyakazi na wateja wetu elimu inayohitajika kujikinga na athari zinazohusiana na kisukari.”

Alisisitiza pia kuwa vipimo hivyo vimeendeshwa na wataalamu na kwa kuzingatia usiri wa taarifa za kiafya kwa wote walioshiriki.

Mbali na uchunguzi wa kisukari, programu ya Exim Cares mwaka huu imefanya pia uchangiaji damu, kuunga mkono tatizo la afya ya akili kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kutoa vifaa vya matibabu, kufadhili na kutoa elimu kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), pamoja na kutoa elimu ya bure kuhusu saratani ya matiti na saratani kwa ujumla. Shughuli hizi zinaonyesha dhamira ya Benki ya Exim katika kuboresha huduma za afya na kusaidia jamii nchini kote.

Kupitia juhudi hizi, Benki ya Exim inaendelea kuthibitisha kuwa uwajibikaji wa kijamii unakwenda zaidi ya uwezeshaji wa kifedha, ukigusa pia ustawi wa afya kwa jamii inayoihudumia. Zoezi hili linaakisi pia maono makubwa ya benki ya kujenga maeneo ya kazi yenye afya na jamii inayojua umuhimu wa kujikinga.

Benki ya Exim na Chama cha Kisukari Tanzania wana matumaini kuwa jitihada hii itahamasisha mashirika mengine kuzingatia afya mahali pa kazi, na hivyo kusaidia jitihada za taifa kupunguza athari za kisukari nchini Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...