Na Janeth Raphael MichuziTv
Waziri Mkuu,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, huku akielekeza lipewe miezi sita ya uangalizi katika kuzingatia miiko, masharti na sheria za uendeshwaji wake.
Sambamba na hilo, ameelekeza kurekebishwa kwa sharti linalotaka kufungiwa kwa nyumba ya ibada iwapo atakosea kiongozi, akisisitiza anayekosea ndiye aadhibiwe bila kuathiri waumini kufanya ibada.
“Natambua ilikuwepo hii moja ya Ufufuo na Uzima kaifungulie, ifungulie wape masharti ya uangalizi ndani ya miezi sita. Ziandikie taasisi zote za kidini kuzikumbusha miiko na mipaka ya ufanyaji kazi, sawa sawa na sheria na Katiba ya nchi yetu,” amesema.
Kanisa hilo lilifutriwa usajili, Juni 2, mwaka huu kutoka na kukiuka masharti ya uendeshaji wake, kwa kuhusisha siasa ndani yake.
Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Novemba 24, 2025 alipozungumza wakati wa mkutano wa hadhara, baada ya ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, 2025.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...