Na Janeth Raphael MichuziTv
Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , Dk Mwigulu Nchemba ameagiza Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na wadau wote wanaohusika wakae na kutengeneza utaratibu wa mpito ili kurejesha huduma za usafiri huo ndani ya siku 10.
Huduma za usafiri wa mabasi hayo zilisitishwa baada ya vurugu za Oktoba 29, mwaka huu zilizosababisha kuchomwa moto kwa vituo vya mabasi na kuharibiwa kwa mifumo ya ukusanyaji nauli na mawasiliano.
Ili kufanikisha urejeshaji huduma kwa mpito, Dk Mwigulu ametaka Wizara ya Ujenzi, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na wadau wengine, wakae na kutengeneza utaratibu.
Ametaka mageti yaliyokuwepo na hayakuwa yanatumika yawekwe na kuanza kurejeshwa masuala ya mawasiliano, umeme na maeneo ya kukusanya mapato na ndani ya siku 10 shughuli zirejee kama kawaida.
“Kaeni kuanzia leo husisheni wadau wote, wakandarasi, mabenki wadau wote kwenye kila eneo ambapo mnaona kuna mmoja wapo anahusika tupate suluhisho la mpito wakati tunaandaa kurejesha katika utaratibu wake wa kawaida,” amesema.
Dk Nchemba ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Novemba 24, 2025 alipozungumza katika mkutano wa hadhara, baada ya ziara yake ya kutembelea miundombinu ya umma iliyoathiriwa na vurugu za Oktoba 29, mwaka huu.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...