Standard Chartered Tanzania imezindua rasmi SC Alumni Association – Tanzania Chapter, ikikusanya pamoja wafanyakazi wa zamani ili kuungana tena, kusherehekea historia yao ya pamoja, na kujenga mtandao imara wa wahitimu utakaendelea kuendeleza urithi na mchango wa Benki.
Hafla ya uzinduzi, iliyofanyika katika Ukumbi wa Marquee wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam, ilikutanisha wahitimu wa Standard Chartered waliowakilisha miaka tofauti, vitengo mbalimbali vya biashara na vipindi tofauti vya uongozi. Tukio hilo lilithibitisha tena dhamira ya Benki katika kuendeleza mahusiano ya muda mrefu na kuimarisha jumuiya ya wafanyakazi wa zamani na wa sasa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Herman Kasekende, Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Standard Chartered Tanzania, alisisitiza umuhimu wa kudumisha mahusiano ya kimaisha na Benki:
“Standard Chartered daima imekuwa zaidi ya sehemu ya kazi — ni nyumbani kwa vipaji, uongozi na malengo ya pamoja. Wahitimu wetu wamekuwa na mchango mkubwa katika kuunda historia yetu hapa Tanzania, na uzinduzi wa leo unaonesha dhamira yetu ya kuadhimisha urithi huo na kuendeleza mahusiano hayo.”
Mwenyekiti wa muda wa SC Alumni Association – Tanzania Chapter, Bw. Erard B. Mutalemwa, pia alisisitiza umuhimu wa jukwaa hilo kama chachu ya ushirikiano endelevu:
“Chama kitatoa fursa kwa wanachama kuungana tena, kufanya mitandao ya kitaaluma, kushirikiana na kupata manufaa maalum. Zaidi ya yote, kinatoa nafasi ya kusherehekea safari zetu, kupeana moyo, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania.”
SC Alumni Association itakuwa kitovu cha:
• Shughuli za mitandao ya kitaaluma na ukuzaji wa ujuzi
• Ufikiaji wa matukio maalum ya wahitimu na mijadala ya kitaaluma
• Fursa za mchango kwa jamii na shughuli za kujitolea
• Uunganishwaji wa kimataifa kupitia mtandao mpana wa wahitimu wa Standard Chartered
Hafla ya uzinduzi ilijumuisha shughuli za ushirikiano, hotuba za wageni rasmi, uzinduzi wa ishara ya chama, na chakula cha jioni kilichounganisha vizazi vya wahitimu ambao kwa pamoja wamesaidia kuunda urithi wa zaidi ya miaka 100 wa Standard Chartered nchini Tanzania.
Chama pia kitaendesha majukwaa ya kidijitali kusaidia usajili endelevu wa wanachama, matukio yajayo, na shughuli za kuwahusisha wahitimu mwaka mzima.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...