Na Mwandishi Wetu London

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Qatar leo, tarehe 24 Novemba 2025, zimesaini hati ya makubaliano (MoU) ya kutambuliana vyeti vya mabaharia katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika jijini London. Hafla hiyo imefanyika pembezoni mwa mkutano wa 34 wa Baraza Kuu la Shirika la Bahari Duniani na kuhudhuriwa na viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya bahari.

Kwa upande wa Tanzania, makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick Salum, huku Mhandisi Abdulaziz Abdullah Al-Sulait, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi wa Qatar, akisaini kwa niaba ya nchi yake.

Kupitia MoU hii, pande zote mbili zinatarajia kuboresha viwango vya umahiri, usalama na ubora katika taaluma ya ubaharia, sambamba na kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar.

Hatua hii inatarajiwa kuongeza ajira kwa mabaharia wa Kitanzania katika meli zilizosajiliwa au kuendeshwa na kampuni za Qatar, kwani hawatalazimika kupitia upya taratibu za uthibitishaji wa vyeti pamoja na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usafirishaji baharini kati ya nchi hizo mbili.

Aidha makubaliano haya yatawezesha mabaharia kupata maslahi bora na fursa zaidi za kazi kwenye masoko yenye ushindani wa juu na kunachochea uhamishaji wa ujuzi na utaalamu wa kimataifa, kwa kuwa mabaharia watafanya kazi katika majukwaa yenye viwango vya juu vya teknolojia na usalama pamoja na kuimarisha uwezo wa Tanzania katika utoaji wa mafunzo ya ubaharia, kwani vyuo na vyeti vyake vitakuwa na uhalali mpana zaidi kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick  Salum na Mhandisi Abdulaziz Abdullah Al-Sulait, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi wa Qatar, akisaini kwa niaba ya nchi yake  wakisaini Hati ya kutambuliana vyeti vya Mabaharia na Qatar katika hafla iliyofanyika London

Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Malick  Salum na Mhandisi Abdulaziz Abdullah Al-Sulait, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi wa Qatar wakiwa wameshikana mkono mara baada kusaini Hati ya Makubaliano ya  kutambuliana vyeti vya Mabaharia na Qatar katika hafla iliyofanyika London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...