Na Mwandishi Wetu

Wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wameaswa kuwa utaalam walioupata kwenda kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa Fedha Elijah Mwandumbya aliyemwakilisha Waziri wa Fedha, Khamis Mussa Omary katika Mahafali ya 51 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema serikali imedhamiria kuwekeza zaidi katika miundombinu na maboresho ya mitaala, ili kuhakikisha vyuo vinatoa elimu yenye ubora unaotakiwa katika karne ya sasa.

Mwandumbya amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu ya juu kutokana mahitaji yaliyopo ili kuhakikisha taifa linakuwa na rasilimali watu yenye ujuzi unaoendana na maendeleo ya teknolojia.

Amesema kuwa Soko la ajira ni pana ambapo wahitimu ni fursa ya kutumia soko hilo katika katika kujiajiri badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa kutokana na changamoto kubanwa kwa ajira na sio Tanzania bali ni Dunia nzima.

“Tuko kwenye mapinduzi makubwa ya teknolojia, hivyo tunahitaji wahitimu watakaoweza kujibu changamoto za uchumi wa kidijitali,” alisema.

Hata hivyo amesema uongozi wa IFM umeendelea kufanya mageuzi ya kitaaluma kwa kuanzisha kozi mpya ili kuandaa wataalamu watakaohitajika kwenye sekta mbalimbali kwenda kutatua changamoto zilizipo katika jamii.

Amesema kuwa katika teknolojia ya mawasiliano ni kazi ya wahitimu kutumia teknolojia hiyo katika kutengeneza fursa na sio kufanya vitu ambavyo vinakwenda kuharibu taaluma.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Emanuel Mjema amewahimiza wahitimu kuwa na uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwaa

Profesa Mjema amewataka wahitimu kutumia fursa ya elimu waliopata katika kutatua changamoto katika jamii ili kuonyesha matokeo ya elimu walioipata chuo cha IFM .

Aidha amesema kuwa Chuo kimakabiliwa na changamoto ya miundombimu ambapo wanaiomba Serikali kusaidia katika kujenga miundombinu hiyo ikiwemo vyumba vya madarasa.

Mkuu wa Chuo cha IFM Profesa Josephat Lotto amesema kuwa idadi ya wanaojiunga chuo imekuwa ikiongezeka kila mwaka na hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa mahitaji katika jamii.

Amesema kuwa Chuo kimeongeza kozi kutokana na mahitaji yaliyopo sasa katika sekta ya fedha inayohitaji kuzalisha wataalam wengi wenye ujuzi.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...