Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori imeendesha mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza na Bodi ya Wadhamini pamoja na VGS

Akifungua mafunzo hayo, PGO, CR Pallage Kauzeni Afisa Wanyamapori Mkuu akimuwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.

Pia ameeleza nia ya Serikali ni kuhakikisha uhifadhi wa wanyamapori unakuwa ni wenye tija kwa taifa na kuleta maendeleo kwa mwananchi mmojammoja.

Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii yakihusu masuala ya usimamizi wa WMA, majukumu ya AA, VGS na bodi ya Wadhamini, utatuzi wa migogoro, masuala ya intelijensia katika uhifadhi, sheria na mikataba, utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika WMA, na migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Mafunzo yameanza jumatatu tarehe 24 na yatahitimishwa tarehe 25 Novemba 2025, Mkoani Iringa katika ukumbi wa Kilimo ni Siasa na yamehudhuriwa na jumuiya kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo jumuiya za Kimbanda, kisengule na Chingoli (Ruvuma), Iluma (Morogoro), ISAWIMA (Tabora) pamoja na Mpimbwe kutoka Katavi.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...