Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wamepongezwa kwa kuendesha Baraza la Wafanyakazi lenye tija ambalo ni kichocheo muhimu cha maamuzi makubwa ya kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, wakati wa ufunguzi wa Baraza la Kwanza la Wafanyakazi la TCAA kwa mwaka wa fedha 2025/2026, lililofanyika Novemba 28, 2025, jijini Dar es Salaam.

Bw. Msangi alisisitiza umuhimu wa vikao vya Baraza la Wafanyakazi katika kuimarisha misingi ya demokrasia sehemu za kazi na kuimarisha mawasiliano kati ya menejimenti na watumishi, huku akiwataka wajumbe kuwasilisha mrejesho kwa watumishi wenzao ili kukuza mshikamano na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

“Baraza hili ni jukwaa muhimu la kujadili na kupanga mwelekeo wa taasisi. Ni chombo cha kuleta maboresho ya kweli ya mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma. Ni wajibu wetu kuhakikisha kila mtumishi anashirikishwa na anapata nafasi ya kuchangia safari ya maendeleo ya TCAA,” alisema Bw. Msangi.

Aidha, alieleza kuwa menejimenti itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kila mtumishi aweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi, ubunifu na uwajibikaji, sambamba na mabadiliko ya teknolojia na matarajio ya sekta ya anga.

“Menejimenti inatambua mchango wa kila mmoja wenu. TCAA inajengwa kwa juhudi za pamoja. Tushirikiane na kuendelea kuunga mkono mipango na malengo ya taasisi ili kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwa Watanzania na wadau wa sekta ya anga,” aliongeza.

Baraza la wafanyakazi lina lengo la kuimarisha mawasiliano ya wazi kati ya menejimenti na watumishi, kujadili mikakati ya kuboresha huduma, mazingira ya kazi, na kuimarisha ufanisi wa taasisi.Watumishi TCAA wapongezwa kwa kuwa na Baraza lenye viwango

Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wamepongezwa kwa kuendesha Baraza la Wafanyakazi lenye tija ambalo ni kichocheo muhimu cha maamuzi makubwa ya kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, wakati wa ufunguzi wa Baraza la Kwanza la Wafanyakazi la TCAA kwa mwaka wa fedha 2025/2026, lililofanyika Novemba 28, 2025, jijini Dar es Salaam.

Bw. Msangi alisisitiza umuhimu wa vikao vya Baraza la Wafanyakazi katika kuimarisha misingi ya demokrasia sehemu za kazi na kuimarisha mawasiliano kati ya menejimenti na watumishi, huku akiwataka wajumbe kuwasilisha mrejesho kwa watumishi wenzao ili kukuza mshikamano na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

“Baraza hili ni jukwaa muhimu la kujadili na kupanga mwelekeo wa taasisi. Ni chombo cha kuleta maboresho ya kweli ya mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma. Ni wajibu wetu kuhakikisha kila mtumishi anashirikishwa na anapata nafasi ya kuchangia safari ya maendeleo ya TCAA,” alisema Bw. Msangi.

Aidha, alieleza kuwa menejimenti itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kila mtumishi aweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi, ubunifu na uwajibikaji, sambamba na mabadiliko ya teknolojia na matarajio ya sekta ya anga.

“Menejimenti inatambua mchango wa kila mmoja wenu. TCAA inajengwa kwa juhudi za pamoja. Tushirikiane na kuendelea kuunga mkono mipango na malengo ya taasisi ili kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwa Watanzania na wadau wa sekta ya anga,” aliongeza.

Baraza la wafanyakazi lina lengo la kuimarisha mawasiliano ya wazi kati ya menejimenti na watumishi, kujadili mikakati ya kuboresha huduma, mazingira ya kazi, na kuimarisha ufanisi wa taasisi.
Picha ya pamoja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kufunguzi wa  mkutano wa kwanza wa Balaza la wafanyakazi wa Mwaka wa Fedha 2025/2026 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...