Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma 

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Maryprisca Mahundi amesema kuwa hadi kufikia Novemba 28,2025 zaidi ya Bilioni 9 wa kuwezesha wananchi kiuchumi zimetolewa na kuwafikia wanufaika zaidi ya elfu 4.

Pamoja na Wizara kuendelea na zoezi la utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa walengwa wanaokidhi masharti na vigezo vya kukopesheka kwa kutumia vitambulisho vya mabenki.

Naibu Waziri ameyaeleza hayo leo Jijini Dodoma Novemba 27,2025 wakati akizungumza na wana Vikundi vya kijamii vya kusaidiana wakiwemo wafanya biashara ndogo ndogo katika Mtaa wa Chilwana Kata ya Ihumwa-Dodoma. 

"Wizara inaratibu na kusimamia jukumu la kuwezesha kiuchumi wafanya biashara ndogo ndogo na vilevile kwa kutumia vitambulisho vya mabenki tunaendelea na zoezi la utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa walengwa wanaokidhi masharti na vigezo vya kukopesheka".

"Ambapo hadi kufikia Novemba 28,2025 zaidi ya Bilioni 9 zimeweza kutolewa na wanufaika zaidi ya elfu 4 wameweza kupata hivyo kama bado hujafikiwa wakati ni sasa".

Aidha Naibu Waziri amesema zipo fursa zingine za kuinua wananchi kiuchumi ambapo jumla ya mifuko  na programu 75 zimeanzishwa na kati ya hizo 63 ziko Serikalini na 12 ziko chini ya Zekta binafsi ambapo mifuko hiyo inaratibiwa na Serikali ili kuhakikisha makundi maalum yanafikiwa na kunufaika".

Akizungumzia suala la malezi na makuzi kwa watoto amesema kuwa familia ni chanzo cha jamii hivyo ni lazima kuitambua na kuienzi kwani hii ni Taasisi muhimu na kubwa katika jamii na ina majukumu makubwa ambayo yanasimamia malezi mema na makuzi kwa watoto sambamba na jukumu la kuhakikisha inalinda mila na desturi zilizo nzuri kwa wato kwa kizazi hadi kizazi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema kuwa, kuwa na vikundi vya uzalishaji peke yake haitoshi kama suala la Malezi na makuzi kwa watoto halitosimamiwa vizuri kwani bado kutakuwa na changamoto ndio maana wameona vema kuvijengea uwezo vikundi hivyo juu ya malezi na makuzi ya watoto.

Leo vimekutana jumla ya vikundi 17 kuangazia fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya Wizara hiyo pamoja na kukumbushana suala la Malezi na Makuzi kwa Watoto.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...