Benki ya Stanbic Tanzania imetoa zawadi za msimu wa sikukuu kupitia kampeni inayoendelea ya Masta wa Miamala.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyoambatana na semina kwa vijana kutoka taasisi mbalimbali, Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Stanbic, Emmanuel Mahodanga alisema "Kampeni hii ya miezi mitatu inalenga kuongeza matumizi ya njia mbalimbali za malipo za benki ya Stanbic kuanzia kadi za Visa, ATM na mtandao smart App wenye zaidi ya mawakala 600, Internet banking na USSD *150*29#".

Aliongeza kusema huduma hii imebuniwa si tu kwa ajili ya kukuza matumizi ya kidigitali bali kuwahamasisha wateja wasiotumia akaunti zao ili kuwapatia nafasi kufurahia urahisi na usalama wa miamala isiyo na fedha taslimu.

Alihitisha kusema: “Tunaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kudumu ya kutembea na wateja wetu kwa kushiriki nao pamoja katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo simu, friji, microwave na pesa taslimu.” Washindi walitoka taasisi mbalimbali zikiwemo GSM, TBL, BLUE COAST, KPMG na PWC.


Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Stanbic, Emmanuel Mahodanga akizungumza na vijana kutoka KPMG wakati wa semina ya promosheni ya Masta wa Miamala iliyofanyika jijini Dar es salaam ikiwa sehemu ya kuwaelemisha namna washindi wanavyopatikana kupitia promosheni hiyo.







Meneja wa Maendeleo ya Biashara kwa Wateja Binafsi wa Benki ya Stanbic, Alice Gamba (kulia) akimkabidhi zawadi microwave, Mike Kabero kutoka kampuni ya PWC mshindi wa promosheni ya Masta wa Miamala ikiwa ni sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu. Jinsi ya kushiriki fanya miamala kwa kutuma pesa kwa uwapendao kwa kutumia huduma za malipo kwa mtandao wa stanbic utaweza kuingia kwenye droo ya kujishindia zawadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...