Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza familia, viongozi, wabunge na waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Joakim Mhagama, iliyofanyika katika Kanisa la Mwenyeheri Maria-Theresa Ledochowska, Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. 

Rais Dkt. Samia alieleza masikitiko makubwa ya Taifa kufuatia msiba huo, akimwelezea marehemu kuwa alikuwa kiongozi jasiri, mwaminifu na mlezi wa viongozi wengi ndani ya Bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyelitumikia Taifa kwa moyo wa kujitoa, nidhamu, uadilifu na hofu ya Mungu, akisimama imara kutetea haki, maendeleo na usawa wa wananchi. 

Aidha, alitambua mchango mkubwa wa Marehemu akihudumu kwa ufanisi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali na Chama cha Mapinduzi, sambamba na uwezo wake wa kubeba majukumu mazito kwa weledi. 

Akigusia urithi wa uongozi aliouacha, Rais Dkt. Samia alisisitiza kuwa moyo wake wa kujali maslahi ya Taifa ndio nguzo kuu ya kumbukumbu ya Hayati Jenista Mhagama, na kutoa wito kwa wabunge na viongozi wote kuiga mfano wake wa maadili na uwajibikaji aliouonesha. 

Halikadhalika, Rais Dkt. Samia aliwataka viongozi kuuenzi mchango wa Marehemu kwa kuimarisha misingi ya uwajibikaji, mshikamano wa kitaifa na utumishi unaolenga maslahi mapana ya wananchi.

 Rais Dkt. Samia alitoa pole kwa familia, ndugu, wananchi wa Jimbo Peramiho, Bunge na Taifa kwa ujumla, na kumuomba Mwenyezi Mungu awape faraja, nguvu na amani, huku akiiombea roho ya Marehemu pumziko la amani ya milele.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...