Wananchi wanaoishi kanda ya ziwa wametakiwa kuchangamkia fursa ya elimu kwa kuwapeleka watoto katika chuo cha usimamizi wa Fedha IFM kampasi ya geita kilichopo wilayani Chato.
Hayo yamesemwa na mhadhiri na mkurugenzi wa IFM kampasi ya Geita Emmanuel Mtani wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya kuhitimu nganzi ya Astashahada chuoni hapo.
Mtani alisema kuwa kutokana na uhaba wa vyuo katika kanda hii ni vyema wananchi wakachamkia fursa hii iliyokuja karibu yao.
"Ni kweli kwamba kuna ghalama kubwa unapomsafirisha kijana kutoka Geita mpaka Dar es salaam jwa ajili ya kutafuta taaluma ile ile ambayo angeipata mahali hapahapa" alisema Mtani
Kampasi ya IFM wilayani Chato ilianza muhula wake wa masomo mnamo November 2024 ambapo ilifanikiwa kudahili wanafunzi 41 ambapo kwa mwaka wa masomo 2025-2026 imefanikiwa kudahili wanafunzi 76.
Mkuu wa wilaya ya Chato Luis Bura ametoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa programu ya shahada katika chuo hicho cha usimamizi wa fedha ili kusogeza elimu ya juu katika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa kuwepo kwa programu ya shahada chuoni hapo kutasaidia kupunguza gharama kutokana na wanaohitaji kusomea programu hiyo kwenda mikoa ya mbali kufata vyuo.
Nao wanafunzi waliohitimu katika kampasi hiyo wamekiri uwepo wa walimu wa kutosha pamoja na mazingira bora ya ya kusoma na kujifunza.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...