Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imeshiriki kikamilifu katika Mkutano wa 20 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (Convention on International Trade in Endangered Species of wild Fauna and Flora - CITES CoP20), kuanzia Novemba 24 hadi Disemba 5, 2025, jijini Samarkand, nchini Uzbekistan.
Mkutano huo, ulihudhuriwa na zaidi ya washiriki takribani 3,000 kutoka nchi wanachama 160, ukihusisha Taasisi za Kiserikali na wadau wa Maendeleo. Tanzania iliwakilishwa na ujumbe kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Idara ya Wanyamapori (WD), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI).
Akifungua mkutano huo Bw. Aziz Abdukhakimov Mgeni rasmi na Mshauri wa Rais wa Uzbekistan kuhusu Mazingira na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ikolojia na Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza nchi wananchama kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira, kupanua maeneo yaliyohifadhiwa na kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori na mimea.
Akiangazia mageuzi ya hivi karibuni nchini Uzbekistan ambayo yameweka uhifadhi wa mazingira kama kipaumbele kwa Serikali, alitoa wito kwa washiriki kutumia teknolojia, ikiwemo Akili Unde (AI) katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za uhifadhi na biashara ya wanyamapori na mimea.
Mkutano wa CoP20 ulijadili ajenda 114 na mapendekezo 51 yanayohusu spishi mbalimbali kama tembo, chui, fisi, papa, taa, mijusi, majongoo bahari, vinyonga, pamoja na miti ya thamani kama vile mpingo, mninga na mkongo. TAFORI katika kutimiza jukumu lake kama Mamlaka ya Kisayansi ya CITES ilichangia mijadala muhimu kuhusu usimamizi endelevu na ulinzi wa spishi za mimea.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI, Dk. Revocatusi Mushumbusi alishiriki katika Mkutano huu akiambatana na Mkurugenzi wa Utafiti, Dkt. Chelestino Balama ambaye huiwakilisha Tanzania katika Kamati ya Mimea ya CITES kama mjumbe kutoka Kanda ya Afrika. Katika Mkutano huo TAFORI ilitoa mchango mkubwa katika kujadili, kuunga mkono ajenda na mapendekezo kuhusu spishi za mimea ambazo zimeonekana kuwa na maslahi mapana kwa nchi.
Ushiriki wa Taasisi katika Mkutano huu ulikuwa muhimu katika kuimarisha msimamo wa pamoja wa Tanzania kwa baadhi ya ajenda hasa katika mijadala ya kanda ya Afrika na kuendelea kutetea maslahi mapana ya nchi katika maeneo ambayo nchi inanufaika na biashara ya kimataifa kupitia maliasili za wanyamapori na mimea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...