Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Islamic Vocational Training Centre (IVTC) kilichopo Unguja Darajani, Zanzibar, kinatarajia kuwapatia elimu ya lishe wanawake wajazito zaidi ya 12,000 kwa lengo la kusaidia watoto wanaozaliwa kuwa na afya njema pamoja na kinga imara dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Akizungumza kuhusu mpango huo, Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. David Msuya, amesema semina za elimu ya lishe zitaanza rasmi Februari 10, 2026 kisiwani Pemba, ambapo kutafanyika mikutano mitatu mfululizo kwa walengwa.
“Baada ya Pemba, tutahamia kutoa semina hizi kwa wakazi wa Kisiwa cha Unguja, na utekelezaji wake utafanyika kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya afya,” amesema Dkt. Msuya.
Ameeleza kuwa maandalizi ya awali yamekamilika na kilichosalia ni kupata maelekezo rasmi kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, ambayo itatoa wataalamu watakaoshirikiana na chuo hicho katika kutoa elimu hiyo kwa ufanisi.
Dkt. Msuya ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo visiwani Zanzibar, mradi huo utaendelea kutekelezwa Tanzania Bara, ukihusisha Mikoa ya Pwani ,Morogoro na pamoja na Iringa




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...