Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 21, 2025 amekagua hali ya bandari ya Barazani mkoani Lindi na kuiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania kukamlisha kwa haraka michakato ya awali ya kitaalam ya ujenzi wa mradi wa Bandari ya Ngongo wilayani Lindi mkoani Lindi.
Amesema kukamilika kwa bandari ya Ngongo kutasaidia kuwaondolea adha watumiaji wa bandari inayotumika sasa ya Barazani ambayo hali yake haiendani na mahitaji ya sasa.
Dkt. Mwigulu ameongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Ngongo kutaleta chachu ya maendeleo mkoani humo kwani bandari ya Lindi imeanza kuchangamkiwa na wafanyabiashara, wakiwemo wa nchi jirani.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...