NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani imeweka mipango madhubuti na kujipanga vilivyo ambayo itaweza kusaidia kwa kiwangon kikubwa katika kuhakikishwa kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi (VVU) hususan kwa upande wa maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanapungua kwa kiwango kikubwa.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa huduma za ukimwi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr. Mariam Nganja kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji Dr. Rogers Shemwelekwa wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya mwendapole na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wakuu wa idara watumishi wa afya pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali.
Mratibu huyo amesema kwamba katika kutekeleza mipango hiyo ya kupunguza maambukizi ya VVU amewahimiza wananchi wote kujenga tabia ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kufahamua hali ya afya zao ikiwemo kufahamu na kujua utambuzi kama wameambukizwa lengo ikiwa ni kuanza kupatiwa dozi ya matibabu kwa haraka.
Aidha amebainidha kwamba kwa sasa hali ya maambukizi wa wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha bado yapo juu hivyo kunahitajika juhudi za makusudi ikiwemo kukemea vikali vitendo vya ubakaji,ilawiti,ukatili wa kijinsia pamoja na baadhi ya tabia ambazo zinapelekea tabia ya maambukizi ya ugonjwa wa VVU.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa Halmashaurii ya Manispaa ya Kibaha Mrisho Mlela ambaye ndiyr aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amewataka wananchi wote kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kutokomeza maambukizi mapya ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi.
Pia amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika Halmashaurinya Kibaha amabazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo amabzo zimeweweza kugusa katika sekta tofauti tofauti ikiwemo suala la kuboresha afya.
Pia amebainisha kwamba Rais katika kuhakikisha anaboresha huduma ya afya kwa wananchi ameweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Liulanzi ikiwa sambamba na kununua vifaa tiba amabvyo vimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwasogezea huduma ya upapatikanaji wa huduma.
Naye Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dr.Abdulkadri Sultan ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuimarisha miundomibu katika vituo vya afya, zahanati pamoja na hospitali ikiwemo suala la upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na madawa kwa ajili ya wananchi.
Maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani katika Halamshauri ya Manispaa ya Kibaha yamefanyika katika viwanja vya mwendapole ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu inasema kwamba shinda vikwazo imarisha mwitikio tokomeza ukimwi kwa mwaka 2025.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...