Kamati ya Madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, imempitisha Diwani wa Kata ya Njiapanda, John Meela kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi kwa kupata kura 34 kati ya kura 45 zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo, katibu wa CCM Wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhan Mahanyu alisema katika uchaguzi huo, Meela alikuwa akigombea na Diwani wa Kahe Mashariki Kulwa Mmbando aliyepata kura 10 na Filbert Shayo wa kata ya Marangu Magharibi aliyepata kura moja.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti, Mahanyu amemtangaza Diwani wa Mwika Kaskazi  Samuel Shao kuchaguliwa kugombea nafasi hiyo kwa kupata kura 33 akiwashinda diwani wa Kirua Vunjo kusini aliyepata kura saba na diwani wa Kibosho kati  kura tano.



 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...