MWENYEKITI wa Bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Stephen Wasira, amewataka vijana nchini kutokubali kutumika na watu wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania kwa kisingizio cha kudai haki, akisema vitendo hivyo vina athari kubwa kwa ustawi wa taifa.
Akizungumza katika Mahafali 10 ya Chuo hicho Kampasi ya Zanzibar amesema kuwa ingawa Tanzania haina adui wa moja kwa moja, kuna baadhi ya mataifa ambayo hayapendezwi na kasi ya maendeleo ya taifa.
“Tanzania haina adui rasmi, lakini si kweli kwamba dunia nzima watu wanatupenda. Kuna wengine wakiona tunapiga hatua wananuna,” alisema.
Wasira alieleza kuwa baadhi ya mataifa hayafurahishwi na jitihada za Tanzania za kujitegemea kiuchumi, kwa kuwa kujitegemea kutaiwezesha nchi kuondokana na utegemezi wa misaada kutoka nje.
“Wengine wangependa wakati wote tuendelee kuwa ‘spoon fed’ kusubiri misaada. Hawapendi kuona tunajitegemea,” aliongeza.
Akitolea mfano maeneo ya maendeleo yanayowatia wasiwasi baadhi ya mataifa, Wasira alisema mafanikio makubwa katika ujenzi wa reli, kuimarika kwa TAZARA na juhudi za kuunganisha Tanzania na mataifa jirani kwa miradi ya kimkakati ni ishara kuwa nchi inajenga msingi madhubuti wa kuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.
“Wakisikia tunajenga reli kutoka Mtwara kwenda Mbambabay, au kuunganisha Tanga na Musoma, wanajua tutakuwa kitovu cha maendeleo kwa eneo lote. Hatuna ugomvi na mtu, lakini sio wote wanafurahia kutuona tunajisimamia,” alisema.
Wasira alihitimisha kwa kusisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda amani na kuepuka kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi au ajenda za kuvuruga nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...