Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Abdul-Razaq Badru amezipongeza timu za Mamlaka hiyo zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya serikali na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kuendelea kulinda na kutangaza taswira ya taasisi hiyo kupitia sekta ya Michezo.

Akitoa salamu  alipotembelea timu hiyo kwa niaba  Kamishna Badru, Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma bwana Hamis Dambaya amesema menejimenti ya Ngorongoro imeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na timu hizo katika mashindano hayo na kulitangaza shirika kupitia utalii wa michezo (sport tourism) 

Katika mashindano hayo Ngorongoro imefanikiwa kutwaa Medali saba huku ikidhihirisha upekee wake kimataifa na kuendelea kuwa _Premium Safari Destination.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...