Na Farida Mangube, Morogoro

Tanzania imetajwa kuwa na fursa kubwa ya kuongeza usalama wa chakula na kukuza uchumi kupitia sekta ya kilimo endapo wakulima watahamasika kulima kilimo cha kisasa kinachojali mazingira kwa kutumia teknolojia mahiri zinazowezesha uzalishaji mkubwa kwenye eneo dogo katika kipindi ambacho mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuathiri sekta ya kilimo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na wataalam pamoja na wadau mbalimbali wa kilimo, mazingira, uchumi, mifugo na mipango ya maendeleo waliokutana mjini Morogoro kwa lengo la kujadili kupitia mradi wa uchumi wa kijani jumuishi (Inclusive green economy – IGE) unaotekelezwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ufadhi wa shirika la misada

Mradi huu umejikita kutoa uelewa kwa wakuu wa idara ambao wanatunga na kusimamia sera ambao wanapatiwa mafunzo ya namna gani wanatumia sera zilizopo kueleta maendeleo bila ya kuharibu mazingira

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Uchumi na Biashara wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Innocensia John, amesema njia sahihi ya kuendeleza kilimo cha kisasa kinachojali mazingira ni kuwahamasisha wakulima kupanda mazao yanayohimili ya ukame kama mikunde, mtama na mihogo pamoja na kutumia teknolojia za kuongeza tija.

“Endapo wakulima wataendelea kupanda mazao ya asili yenye uwezo wa kustahimili ukame, watakuwa na uhakika wa chakula na pia watazalisha mazao mengi katika eneo dogo. Hii ndiyo njia sahihi ya kujenga ustahimilivu kwenye kilimo,” alisema Dkt. Innocensia.

Aidha asemema mabadiliko ya tabianchi yameongeza hitaji la kubadili mfumo wa uzalishaji ili kulinda mazingira na kuzuia upotevu mkubwa wa mazao ambao kwa sasa unaathiri uwezo wa nchi kuzalisha vya kutosha.

Kwa upande wake, Dkt. Aloyce Hepelwa Msimamizi wa Mradi wa IGE kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema mradi huo unalenga kuziwezesha jamii kutumia rasilimali kwa tija bila kuathiri mazingira, ikiwa ni sehemu ya kuunganisha kilimo cha kisasa na ujenzi wa uchumi wa kijani.

“Mradi wa IGE umejikita katika kuwezesha jamii kupitia watunga sera kutumia rasilimali kwa tija bila kuathiri mazingira. Tunatarajia kuona ongezeko la uzalishaji, uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya ardhi ifikapo mwisho wa mradi,” alisema Dkt. Hepelwa.

Mradi huo utakamilika mwaka 2027 una nafasi ya kuchochea mageuzi ya kilimo nchini kwa kuongeza maarifa, kubadili mtazamo wa vijana kuhusu kilimo cha kisasa na kuimarisha maamuzi ya sera kwa ushahidi wa kitaalamu.

Bw. Vedastus Sitta ni mwakirishi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, amesema kuwa kilimo mahiri ni sehemu muhimu ndani ya mpango mpana wa mageuzi ya kilimo unaobebwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na mpango wake wa miaka 25 utakaonza 2026 hadi 2051.

“Kilimo mahiri ni eneo dogo lakini muhimu katika mageuzi ya kilimo ambayo dira imeyabainisha. Bila kilimo cha kisasa kinachozingatia utunzaji wa mazingira, hatutaweza kuongeza uzalishaji, kuwaingiza vijana wengi kwenye kilimo au kupanua mauzo yetu nje ya nchi,” alisema Sitta.

Amesema hatua zinazochukuliwa na taasisi kama UDSM kupitia mradi wa IGE zinaonesha kuwa utekelezaji wa dira umeanza kabla ya muda, jambo linalotoa matumaini ya kujenga taifa lenye uchumi shindanishi, jumuishi na linalotumia ardhi kwa tija.

“Nawapongeza wadau wote kwa kuanza utekelezaji kabla ya muda rasmi. Tunaomba vijana kujitokeza kwenye kilimo cha kisasa kinachotumia eneo dogo kuzalisha zaidi ili taifa lipate chakula cha kutosha na kuongeza pato la kigeni,” aliongeza.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...