Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amekutana na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kuwapongeza kwa jitihada wanazoendelea kufanya katika utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini.

Mkutano huo umefanyika tarehe 8 Desemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa TPDC jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kujadili mikakati ya TPDC.

Pamoja na mambo mengine Mhe.Salome ameelekeza Menejimenti ya TPDC kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia majumbani na ujenzo wa vituo vya gesi asilia kwenye vyombo vya moto (CNG) ili Watanzania waendelee kunufaika zaidi na rasilimali hiyo muhimu.

Aidha, amesisitiza kuwa miradi ya utafiti na uendelezaji wa gesi asilia, ikiwemo mradi wa LNG kuanza kushika kasi baada ya majadiliano kukamilika ili kuongeza tija katika uwekezaji na kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na rasilimali zake.

Katika hatua nyingine, Mhe.Naibu Waziri ameipongeza TANOIL ambayo ni kampuni tanzu ya TPDC kwa kuendelea kuwekeza kwenye biashara ya mafuta huku ikiwakilisha Kampuni ya kizawa lakini pia kuendelea kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha muda wote.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...