Na Mwandishi wetu

TANZANIA imeandika historia nyingine kubwa katika nyanja ya kidiplomasia na utamaduni baada ya kufanikiwa kupitisha ajenda ya kuanzishwa kwa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (ALHC) kama Taasisi rasmi ya Umoja wa Afrika (AU), kitakachokuwa na makao yake nchini Tanzania.

Ushindi huo umepatikana katika Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Nchi za Afrika (STC–YCS5) uliofanyika Jijini Bujumbura, Burundi.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (MwanaFA), ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha nafasi ya Tanzania kama mhimili wa ukombozi wa bara la Afrika inatambulika rasmi kwa kuanzishwa kituo hicho.

Katika mkutano huo, MwanaFA alionekana akibadilishana mawazo na kufanya mazungumzo ya kimkakati na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini, Mhe. Gayton McKenzie, Viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili ambazo zina historia ndefu na ya kipekee katika harakati za ukombozi.

Akizungumzia mafanikio hayo, MwanaFA kupitia ukurasa wake wa Facebook ameeleza kuwa wiki hii imekuwa nzuri kwa Tanzania:

"Tumeweza kusimamia kupitishwa kwa ajenda ya Tanzania ya kuanzishwa kwa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika (ALHC) kama Taasisi ya Umoja wa Afrika... Wiki nzuri kwa Tanzania, kama mshiriki mkubwa na muhimu katika Historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika" alisema.

Kuanzishwa kwa kituo hicho nchini Tanzania kunategemewa kuongeza fursa za utalii wa kihistoria na kuimarisha ushawishi wa nchi katika masuala ya utamaduni na diplomasia barani Afrika.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...