Na WAF, Dar es Salaam

Serikali imeiasa jamii katika Bara la Afrika kuunganisha nguvu na kushirikishana katika afua mbalimbali zitakazochangia katika kukabiliana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) kutokana na kukithiri kwa matumizi holela ya dawa za antibiotiki kwa binadamu pamoja na shughuli za ufugaji na kilimo.

Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe Desemba 2, 2025 wakati akizungumza na wanahabari katika maadhimisho ya Wiki ya Kukabiliana na Usugu wa Dawa na matumizi holela ya dawa kwa binadamu, mifugo na kilimo.

"Tunataka tuunganishe nguvu kutoka afua mseto za wadau mbalimbali walio mstari wa mbele kwenye vita hii na kuwa na matumizi sahihi ya dawa kulingana na maelekezo ya wataalam," amesema Dkt. Magembe.

Dkt. Magembe amesema, baadhi ya tafiti zilibainisha uwepo wa matumizi holela ya dawa za binadamu kwenye mifugo na maza, hali inayochangia dawa kutofanya kazi kwa ufanisi na kusababisha matumizi ya dawa yenye nguvu zaidi ili kutibu, hali inayochangia gharama kubwa katika matibabu na wakati mwingine husababisha madhara makubwa kwa binadamu, mifugo pamoja na mazao.

Dkt. Magembe ameongeza kuwa, baadhi ya watu huandikiwa dawa lakini wakinywa siku ya kwanza na ya pili wanaacha hali hiyo inazidi kuongeza usugu wa vimelea vya maradhi na hata kuchochea baadhi vifo kutokana na usugu huo.

Bw. Yuda Sule, akiwa mmoja wa wawasilisha mada katika kongamano hilo, amesema ili malengo ya kukabiliana na usugu ya dawa yafanikiwe ni muhimu kila mmoja ndani ya jamii akaona anawajibu wa kuchukua hatua.










Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...