Na. Jacob Kasiri - Zanzibar.
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kupanua wigo wa uhamasishaji wa utalii na fursa za uwekezaji kwa kusaini makubaliano ya kihistoria na Jumuiya ya Uwekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), hatua inayolenga kuchochea fursa za uwekezaji, kuongeza thamani ya mazao ya utalii na kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kama kitovu cha utalii wa kimataifa.
Makubaliano hayo yalisainiwa leo Desemba 2, 2025 katika hafla iliyoongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt. Aboud Jumbe, ambaye aliipongeza TANAPA kwa juhudi zake za kuanzisha Ofisi Kiunganishi Zanzibar, Ofisi ambayo ndiyo imekuwa kichocheo cha kufanikisha makubaliano hayo.
Dkt. Jumbe alisema, “Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na TANAPA ili kuimarisha mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya utalii hususani ndani ya Hifadhi za Taifa zilizopo Tanzania Bara.”
“Kitendo hiki kitachagiza wageni wengi wanaotokea Zanzibar kuwa na siku nyingi za kukaa ndani ya Hifadhi za Taifa tofauti na ilivyo sasa wageni wengi wanaokwenda kutalii bara hurudi kulaka Zanzibar. Hivyo kwa kuongeza uwekezaji tutakuwa tumefikia malengo ya ZATI ya kuvutia wawekezaji wapya, kuimarisha miundombinu, kupanua huduma bora za utalii na kuongeza ajira”, aliongeza Dkt. Jumbe.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA John Nyamhanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki aliipongeza “ZATI” kwa kuja na mkakati huo wenye lengo la kuongeza kasi ya uwekezaji katika mazao ya utalii na malazi, kwani ongezeko la mazao ya utalii na uwekezaji katika malazi utaongeza siku kwa watalii kukaa (spend) ndani ya hifadhi kutakakokwenda sambamba na ongezeko la mapato kwa TANAPA na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Kamishna Nyamhanga alitanabaisha kuwa TANAPA inasimamia Hifadhi za Taifa 21 zenye vivutio vya kipekee ambavyo vinamchango wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja unaoinufaisha sekta ya utalii Zanzibar na kuchangia katika pato la taifa linalozinufaisha pande zote mbili za muungano.
“Makubaliano hayo yatatoa matokeo chanya hasa katika kuongeza ushiriki wa sekta binafsi, kuboresha taarifa za masoko, na kuimarisha mtiririko wa watalii kutoka katika vivutio vya Zanzibar kwenda nyikani bara. Hali hii itakuza utalii wa fukwe na ule wa nyikani, aliongeza Kamanda Nyamhanga.
Naye, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Ofisi Kiunganishi ya TANAPA - Zanzibar, Dkt. Halima Kiwango alisema, “Makubaliano hayo ni mwendelezo wa kazi kubwa tunayoifanya katika kuimarisha mahusiano na taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sekta binafsi na wadau wa utalii ili kukuza soko la utalii nchini”.
Awali katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa ZATI Suleiman Ali Mohamed alisema, “ZATI imeelekeza nguvu zake za uwekezaji na utaalamu wa masoko ya kimataifa, jambo linalotarajiwa kuongeza kasi ya uwekezaji na kuvitangaza vivutio vya Tanzania bara na Zanzibar kwa watalii wa kimataifa.”
Makubaliano haya ya TANAPA na ZATI yanatarajiwa kuongeza ufikikaji wa taarifa katika masoko ya utalii, kuunganisha mifumo ya taarifa, na kuboresha utalii shirikishi baina ya Zanzibar na Hifadhi za Taifa Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...