Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka ametoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya Vijana nchini kuhakikisha wana takwimu sahihi na changamoto zinazowakabili vijana katika maeneo yao ili kuwa rahisi kuwafikia pamoja na kuhakikisha wanawaunganisha vijana hao na program na fursa zote za Kitaifa zinazohusu ajira,ujuzi na uwezeshaji kiuchumi.

Waziri Nanauka ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Desemba 17,2025 wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri zote nchini.

Na kuwataka pia kuimarisha ushirikiano na wadau wa masuala ya vijana waliopo katika maeneo yao kwa kuwaunganisha na vijana ili kuleta matokeo ya haraka na endelevu huku wakizingatia uwajibikaji,uadilifu na matumizi sahihi ya rasilimali zinazotolewa kwaajili ya vijana zitakazokuja katika maeneo yao.

"Natoa Rai kwenu,katika kutekeleza majukumu yenu hakikisheni mnakuwa na takwimu sahihi za vijana waliopo katika maeneo yenu na changamoto wanazokabiliana nazo pia hakikisheni mnawaunganisha vijana hao na program na fursa zote za Kitaifa na zinazopatikana katika maeneo yenu zinazohusi ujuzi,ajira na uwezeshaji wa kiuchumi"

Aidha Waziri Nanauka amesema kuwa pamoja Serikali ya awamu sita kufanya kila jitihada za kutaka kuwapa sauti vijana lakini bado vijana hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji majibu ya kimkakati na majibu pamoja kwani wapo waliokosa ajira zenye tija,mitaji,masoko kwa shughuli wanazofanya,fursa za kiuwekezaji na pengo kati ya ujuzi wanaopata vijana na mahitaji ya soko la ajira.

Ambapo pia amesema ili kuwafikia vijana wengi zaidi ni lazima wakae kwa pamoja ili kujadiliana na kukubaliana kutokana na yale ambayo wanayafanya na kuyajua katika mazingira ya kazi ili kujua namna wanavyoweza kuunda mkakati wa pamoja.

"Ni muhimu kutambua kuwa vijana wetu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji majibu ya kimkakati na majibu ya pamoja,na changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa ajira au kukosa ajira zenye tija zaidi lakini pia tunakabiliwa na pengo kati ya ujuzi wanaopata vijana katika mifumo yetu ua Kielemu na mahitaji ya soko la ajira".

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Maendeleo ya Vijana Jenifer Omoro amesema kuwa Maafisa Maendeleo wa Vijana ni kiungo muhimu kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa katika kushughulikia masuala ya ya Maendeleo ya vijana na ndio watekelezaji wa Sera,Miongozo,Mikakati,Program na Afua mbalimbali za maendeleo ya vijana hapa nchini.

Na ndio maana kikao kazi hiki kimeandaliwa si tu kwaajili ya kujadiliana bali pia kama jukwaa la kupata mawazo yao wakati ambao pia Wizara inaandaa muundo na mpango mkakati utakaowezesha Wizara na Maafisa Maendeleo ya vijana katika ngazi zote za Mkoa na Halmashauri kutekeleza majukumu ya kuwahudumia vijana kwa ufanisi.

Hiki ni kikao kazi cha kwanza tangu kuanzishwa kwa Wizara hii mpya ya Maendeleo ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais ambacho kimewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Vijana kutoka mikoa yote 26 na Halmashauri 184 za hapa nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...