Na Mwandishi wetu.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwapa mafunzo ya namna bora ya kusimamia masuala ya Itifaki na kuhudumia wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.

Akifungua mafunzo kwa Maafisa Uhusiano kwa Umma  wa Mamlaka  hiyo jijini Mwanza  Mshauri wa Jeshi la Uhifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya ameeleza kuwa ni muhimu kwa kwa maafisa uhusiano kwa umma wa mamlaka hiyo kuendelea kujiimarisha katika masuala ya mawasiliano na itifaki za kijeshi ili kuimarisha utendaji kazi wao na kufikia viwango ambavyo mamkala imejiwekea kwenye mipango yake.

“Tunataka kuendelea kuwa Premium Safari Destination katika taasisi yetu, hivyo ni muhimu kubadilika na kupeana mafunzo ya mara kwa mara kwa kuzingatia ubunifu, maarifa na nidhamu maeneo ya kazi ili wageni tunaowahudumia wafurahie huduma zetu na kuendelea kututangaza maeneo yote duniani”alisema Kanali Machibya.

Kaimu Meneja Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo yeye na timu yake kutasaidia kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho katika kipindi hiki ambacho mamlaka hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa kiutendaji na kihuduma.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa kivutio bora barani Afrika kutokana na umahiri wake katika kusimamia shughuli zote za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii jambo ambalo limekuwa likivutia wageni  wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...