Na Mwandishi wetu


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameendelea Kuwakaribisha Wafanyabiashara na Wawekezaji, kuchangamkia fursa Jijini Dodoma kwa kile alichokisema kuwa Mkoa huo unaendelea kubadilika kimaendeleo kutokana na Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki na fursa za kutosha.

Mhe. Rosemary amesema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Uliofanyika katika Ukumbi wa New Generation Kisasa Desemba 15, 2025 wakati akimuwakilisha Mgeni Rasmi Mhe. Anthony Mavunde Waziri wa Madini.

Mhe Rosemary Amesema kuwa kwa sasa Jiji la Dodoma linavyo Vipaumbele Vitano vya Uwekezaji ambavyo Wafanyabiashara wanakaribishwa kufanya uwekezaji wenye Tija, huku akianisha Vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na Fursa za Kilimo, ambapo amesema kuwa bado Dodoma inayo ardhi kubwa ya kuwekeza kwenye Kilimo na hasa Kilimo cha Umwagiliaji.

Ametaja kipaumbele kingine kuwa ni pamoja na Utalii ukiwemo utalii wa Wanyama, majengo ya Serikali pamoja na Mila na Desturi za Wenyeji (Wagogo).

Sambamba na hilo amesema kipaumbele kingine ni mpangilio wa Ujenzi wa miundo mbinu inayofikika mfano bandari ya Nchi Kavu, Uwanja wa Ndege, na Barabara zinazoingia na kutoka Jijini humo, hivyo ni fursa kwa Wafanyabiashara kupokea na kusambaza mizigo yao Mikoa mingine.

Aidha ameongeza kuwa fursa nyingine ambayo ni kipaumbele kwa sasa, ni Ujenzi wa Viwanda Vikubwa na Mahotel kwakuwa bado yapo maeneo makubwa ya Ujenzi na yanafikika kiurahisi, na maeneo haya yanatolewa bure kwa sharti la mwekezaji kukamilisha Ujenzi ndani ya Mwaka Mmoja.

Kipaumbele cha Tano kimetajwa kuwa ni Sekta ya Madini, ambapo kutokana na utafiti uliofanywa na GST umebaini uwepo wa Madini mengi ya Kimkakati ikiwemo Dhahabu, Nikel, na madini mengine, na kwamba ni fursa kutokana na mnyororo wa thamani wa Biashara hiyo ya madini.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...